FAHAMU MAHAKAMA YA WATOTO INAVYOLINDA HAKI USIKILIZAJI KESI YA MADAI NA JINAI


 Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

HAKIMU wa Mahakama ya Watoto Wilaya ya Temeke Orupa Mtae endapa mtoto atafanya kosa lolote kama kuiba,kubaka,atalawiti ili mradi liwe limeainishwa kwenye kanuni ya adhabu sura namba 16 endapa mtoto atafanya kosa lolote kama kuiba,kubaka,atalawiti ili mradi liwe limeainishwa kwenye kanuni ya adhabu sura namba 16.

Amesema kuwa mahakama ya watoto ipo rasmi kisheria na kwamba inasikiliza nashauri yote yanayo muhusu mtoto pale ambapo amekinzana au amekutana na Sheria.

"Mahakama hii inasikiliza mashauri yote ya madai na jinai,mashauri ya jinai ni pale mtoto anapofanya kosa kinyume na Sheria ya kanuni ya adhabu  huku akisema makosa yote ambayo yameainisha kwenye Sheria ya adhabu pale yanapofanywa na mtoto ndipo tunasema ataletwa katika mahakama ya watoto, tukumbuke mtoto ni yule ambaye yupo chini ya miaka 18," ameeleza endapa mtoto atafanya kosa lolote kama kuiba,kubaka,atalawiti ili mradi liwe limeainishwa kwenye kanuni ya adhabu sura namba 16.

Hakimu huyo ameeleza kuwa katika mahakama hiyo wanaangalia kigezo cha ustawi bora wa mtoto huku akisema mtoto huyo anapofikishwa Mahakamani wanaangalia haki zake za msingi hata kama ni mshitakiwa wanahakikisha  haki zake hazivunjwi.

"Sheria inataka mtoto anapokuwa Mahakamani awa na mzazi,mlezi au mwakilishi ambaye ni wakili wa utetezi na anapokuwa Mahakamani tunahakikisha anakuwa na mtu wa kusaidia katika mambo yote ya kisheria," amesema Hakimu Mtae.

Ameeleza kuwa umuhimu wa kuwa na mzaz,mlezi mahakamani ili jambo lolote linalowekutokea na halielewi  mzazi atamsaidia.

Hakimu Mtae ameongeza kuwa mototo anapokuwa Mahakamani wanasikiliza kesi jinai   wanahakikisha lugha inayotumia ni nyepesi na inaeleweka.

Amesema pia kuana  mambo engine ya kisheria ambayo wanayozingatia ni kuhakikisha mtoto haulizwi amaswali yanayowez kutweza utu wake, yakamfanya akaogopa ili  kumuwekea mazingira ya kumfanya asiogope pamoja na kwamba amefanya kosa ni mshitakiwa aweze kuona haki inatendeka.

"Hakimu Mtae amesema kama ilivyo kwenye mahakama za wakubwa waliona ushahidi umejitosheleza , jamuhuri imefanikiwa kuthibitisha shitaka mtoto huyo atapata nafasi ya kujitetea  na kwamba baada ya hapo hakimu ataandika maamuzi ili kumtia hatiani ama kumuachia huyo endapo ataona kosa halijathibitika upande wa jamuhuri hiyo," ameeleza.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA