MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI

 

Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

WIZARA ya Madini imepanga kununua magari 89 na pikipiki 140 kama sehemu ya uboreshaji wa usimamizi wa Sekta hiyo kupitia Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa hasa kwenye usimamizi wa ukusanyaji wa maduhuli lengo likiwa ni kudhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato na utoroshaji wa maduhuli.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri Madini Anthony Mavunde wakati akizindua magari mapya 25 kwa ajili ya kusambazwa kwenye Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa pamoja na kukabidhi magari hayo kwa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa waliohudhuria uzinduzi huo.

Waziri huyo amesema kuwa magari yote 85 yatakayonunuliwa yatagharimu zaidi ya shilingi bilioni 18.

Waziri Mavunde ameeleza kuwa lengo ni kuboresha Sekta hiyo na kwamba magari hayo yanaenda kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato katika mikoa ya kimadini.

Ameongeza kuwa magari yaliyozinduliwa 25 ni awamu ya kwanza ya magari 89 yanayotarajiwa kuletwa sambamba na pikipiki 140 zitakazosambazwa kwenye ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa zilizopo nchi nzima.

"Hatua hii ni muendelezo wa dhamira ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kuboresha utendaji kazi wa wizara na taasisi zake na katika mwaka huu wa fedha wizara ya madini imepangiwa kukusanya shilingi trilioni moja hivyo vitendea kazi hivi vitasaidia katika kufikia lengo," amesema.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amempongeza Waziri Mavunde kwa jitihada zake za usimamizi wa Sekta ya Madini na kuwataka watendaji wa Tume ya Madini kuhakikisha wanaonesha matokeo chanya kwenye utendaji kazi.

Kwa upande Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema serikali imekuwa ikiongeza bajeti kwa wizara ili kuhakikisha kunakuwa na vitendea kazi vya kutosha.

Amefafanua kuwa vifaa hiovyo vitasaidia kuongeza kasi ya ukusanyi mapato ili kuongeza makusanyo ya serikali.

“Wizara imekuwa na bajeti ya kutosha leo hii tumepokea magari 25 ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika utekeleza ji wa majukumu. Vitendea kazi hivi vitasaidia Maofisa madini wakazi wa mikoa kufuatilia shughulimbalimbvali za madini katika maeneo yao,”amesema.

Kwa upande wake Ofisa Madini Mkazi wa Mererani Nchangwa Marwa ameipongeza serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.

Amesema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa maduhuli ya serikali na kufika maeneo mengi ambayo ilikuwa ni ngumu kufikika.

“Changamoto ya vitendea kazi ilikuwa inakumba maeneo meneo mengi tunaishukuru serikali na tunaamini vitaenda kuongeza chachu na kasi ya ufuatiliaji wa maduhuli ya serikali,”ameeleza.

Wizara ya Madini kwa magari husika amesema kuwa magari yatatumika kama chachu ya Ofisi za Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwenye ongezeko la makusanyo ya maduhuli.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI