WANAFUNZI SHULE YA MSINGI ANGLO JUNIOR WATEMBELEA HIFADHI YA MIKUMI


Na Asha Mwakyonde 

WANAFUNZI wa shule ya msingi Anglo junior iliyopo jijini Dodoma wametembelea,wamefanya Utalii wa ndani katika Hifafhi ya Taifa ya Mikumi kwa lengo la kujifunza na kujionea vivutio vya utalii vilivyopo pamoja na kujifunza kwa vitendo.

Pia uwepo wa treni ya kisasa ya SGR umechochea kuongezeka kwa idadi kubwa ya watalii wa ndani na nje ya nchi ambapo kutoka mwezi Julai hadi Oktoba mwaka huu hifadhi hiyo imehudumia jumla ya watalii 65,000 na kwamba idadi hiyo ni kubwa.

Akizungumza katika hifadhi hiyo hivi karibuni Mkuu wa Kitengo cha Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi,Mhifadhi Mwandamizi wa Uhifadhi Herman Mtei  amesema kuwa kuongezeka kwa idadi hiyo kunatokana na juhudi za Rais Dk Samia Suluhu Hassan za kutengeneza uwanja mkubwa wa ndege ambao umekuwa ni chachu ya kuleta watalii nchini na kutembelea hifadhi ya Mikumi.

" Treni ya ya kisasa ya SGR nayo imekuwa ni sehemu kubwa ya kuongeza watalii wa ndani ambapo siku za mapumziko tunahudumia watalii 1000 kwa siku," ameeleza Mhifadhi huyo.

Mwalimu kutoka shule ya Anglo Junior Innocent Ankunda ameeleza kuwa utalii huo kwa wanafunzi unawajengea kujua mbuga za wanyama zilizopo nchini ikiwa ni pamoja na kuwajengea kumbukumbu za vitu ambayo wameviona na kujifunza kwa vitendo.

" Mwanafunzi anaposoma Anglo Junior sio tu anaishia kusoma darasani masuala ya mbuga na mengine bali anatembelea na kuvishika na kuviona kama mtaala mpya unavyoelekeza hapa nchini," amesema mwalimu Ankunda.

Mwanafunzi wa shule hiyo Sasha Lema amesema kuwa siku hiyo ni nzuri moyoni mwake kutembelea hifadhi hiyo huku akieleza kwamba ameona wanyama wengine ana kwa ana kama pumbamilia naTembo.

Naye Mkurugenzi wa shule ya Anglo Junior ambaye pia ni mbunge Vitu Maalum Mkoa Kagera Anatropoia Theonest alisema kuwa nafasi za kutembelea hifadhi zipo kwa kiwango kidogo kwa watoto, wanafunzi wa kitanzania kuchangia huduma kidogo kwenda kuona vivutio vilivyopo kwenye hifadhi.

"Bila shaka watoto, wazazi wamefurahi nina imani huu ni mwanzo mpya na naamini watakaoona na kusikia watawaleta watoto wao kusoma shule ya Anglo Junior ambayo inafundika kwa vitendo sio darasani tu, tusiache watalii wanaotoka nje ya nchi na sisi tunafurahi kuona wanyama kama Tembo na Simba na wanyama wengine," amesema.

Aidha ameeleza kuwa ni imani yake kwamba ziara hiyo italeta hamasha kwa shule nyingine kuwapeleka wanafunzi wao kuona kwa macho na kujifunza kwa vitendo.

















Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU