Na Mwandishi wetu,Ikungi Singida
UJUMBE wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala (THBUB) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Mohamed Khamis Hamad,umetoa mafunzo kwa Watendaji wa Kata kutoka Kata zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, leo Januari 27, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Halmashauri hiyo.
Aidha, Mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha Watendaji hao namna ya kuheshimu haki za binadamu na kuzingatia misingi ya utawala bora wakati utekelezaji wa majakumu yao ikiwemo kuwashirikisha wananchi katika masuala mbalimbali yanayowahusu.
Pia, Watendaji hao wamepata nafasi ya kuuliza maswali sambamba na kuelezea changamoto wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
0 Comments