NMB IMEPANGA KUWAFIKIA WANANCHI 2000 KUFUNGUA AKAUNTI NMB PESA

Na Asha Mwakyonde,DODOMA 

BENKI ya NMB hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2024, benki hiyo imefanikiwa kuvikia vijiji 1,000 kupitia kampeni ya NMB Kijiji Day lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha kila Mtanzania, popote alipo, anapata huduma za kifedha.

Pia NMB mwaka huu inapanga kuwafikia wananchi 2,000 ili kuwawezesha kufungua akaunti ya NMB Pesa kwa gharama nafuu ya shilingi 1,000 pekee ambapo akaunti hiyo inawapa wateja fursa ya kupata mikopo bila kulazimika kufika katika matawi ya benki.

Hayo yalisemwa na Afisa wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Alfredy Shayo katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma na wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), alieleza hatua hiyo inayochochea ukuaji wa uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.

Alisema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu,Benki ya NMB inatamani kutumia mwezi wa mtukufu wa Ramadhani kuombea uchaguzi uwe wa amani.

Shayo alitoa wito kwa Jumuiya ya ALAT kushirikiana na NMB katika kutoa elimu ya kifedha kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, aliishukuru Benki ya NMB na ALAT, kwa mchango wao katika kuendeleza maendeleo ya mkoa huo na kwamba uwepo wa Jumuiya hiyo jijini Dodoma kwa siku tatu ni fursa kubwa kwa wakazi na wafanyabiashara.

Alisema kuwa ziara ya viongozi wa ALAT katika miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa jijini Dodoma itawawezesha kueleza kwa Watanzania kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa Mkoa huyo aliongeza kuwa NMB na Jumuiya hiyo wanaendeleza ustawi wa Dodoma

Post a Comment

0 Comments

TUENDELEE KUOMBA MUNGU HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA MPOX