ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 2 KUKUSANYWA NA BUNGE MARATHON

Na Asha Mwakyonde, DODOMA 

BUNGE Marathon linatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 2 Aprili 12, mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya sekondari ya wavulana wa kidato cha tano na sita.

Pia watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi katika kushiriki,kushangalia kwa lengo la kujenga elimu ya Taifa la Tanzania pamoja na kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake.

Hayo yamesemwa leo Aprili 10,2025 bungeni na Naibu Spika wa Mussa Zungu mara baada ya kupokea vifaa vya michezo kutoka kwa wafadhili ameeleza kuwa marathon hiyo ni muhimu kwa wadau wa elimu hasa katika Wanafunzi ambao watawapokea na kuwajengea shule hiyo.

"Mimi binafsi nitacheza namba mbili na Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson, atacheza namba moja na msishangae kuona nashiriki na kuchukua ubingwa na kwenye vigezo vitatu vya nusu fainali ya marathon hii ya kilomita 5 na 10" ameongeza.

" Leo tupo hapa kupokea vifaa ambavyo vitatumika siku ya Jumamosi mimi na Katibu wa Bunge tumepokea vifaa hivi, tunawashukuru wafadhili wetu ambao wametufadhili kwa hali na mali kuhakikisha marathon hii inakuwa na sura ya kitaifa na kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia katika masuala ya elimu," amesema.

Ameeleza kuwa eneo la ujenzi wa shule hiyo litaanuliwa baadae na uongozi wa Bunge na kujulishwa wananchi.

Naibu Spika ameeleza kuwa ule utaratibu wa Haji Manara wa kupanda pikipiki anaenda kujitokeza mbele utazuiliwa na kuhakikisha wanawazuia watu watakao vamia na kutafuta ushindi wa magumashi.

Ameongeza kuwa marathon ya Bunge lijalo wataweka utaratibu wa Rais Dk. Samia wa Nishati Safi na salama ili kuunga mkono vizuri kwa sababu Rais huyo ndiye kinara wa Nishati hiyo katika Afrika na hatimaye kutambulika Kimataifa.

Awali Mwenyekiti wa Bunge Sport Festo Sanga amesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 99, na kwamba marathon hiyo itasaidia kujenga shule hiyo ya wavulana.

Aidha alimshukuru Spika wa Bunge Dk.Tulia kwa maono yake ambayo yanaendelea kuzaa jambo kubwa katika Bunge hilo.

Post a Comment

0 Comments

KAMATI MAALUM HUDUMA YA AFYA YAUNDWA MAANDALIZI YA AFCON