Na Asha Mwakyonde
MENEJA Masoko na Uhamasishaji kutoka Mfuko wa Self MF, Linda Mshana ameeleza kuwa wapo katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, ‘Saba Saba’ kwa lengo la kutoa elimu kuhusu fursa mbalimbali za mikopo zikiwamo za Nishati mbadala, mikopo kwa wafanyakazi ya kuboresha makazi yao.
Hayo ameyasema leo Julai 1,2025 jijini Dar es Salaam katika banda la mfuko huo wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema wana mambo mazuri ambayo wamewaletea wananchi yakiwamo huduma mpya za mikopo Nishati mbadala na vikundi ambavyo vimejisajili ambao wanafanya shughuli za ujasiriamali kwa pamoja huku akisema wanatamani wananchi.
"Tupo hapa kwenye viwanja hivi vya maonesho haya kuwatangazia fursa zilizopo katika mabanda yetu," amesema Mshana.
Meneja huyo ameongeza kuwa mikopo hiyo ya Nishati mbadala ambapo wameanza kuitoa mwaka huu na kwamba wao kama Self MF wameona wananchi wanakosa fursa ya mikopo ya Nishati mbadala.
" Tumeona fursa nyingi zinawapita kwa wale ambao hawana dhamana, hawapo katika sehemu ambayo sio rasmi ya biashara tukaona tusiwaache, tunawakaribisha wananchi," amesema.
Amefafanua kuwa wana mikopo ya wafanyakazi wa serikali wanaotaka kuboresha makazi yao,kufanya biashara za aina mbalimbali ambazo ni halali.
Mshana ameeleza kuwa katika banda hilo wanatoa elimu mbalimbali kuhusu mambo ya kifedha, biashara pamoja na ushauri.
"Tunajali maisha ya wananchi be zao, mali zao pamoja na maisha yao tuna wakaribisha wananchi kuja katika banda letu kujionea fursa mbalimbali ambazo tuna zitoa,"amesema Mshana.
Aidha amewashauri wananchi kujitokeza kwa wengi katika banda hilo kwa lengo la kupata elimu ya mikopo hiyo na baadae kufanya uamuzi wa kuomba ili waweze kuendeleza shughuli zao za kujiingizia kipato.
0 Comments