Na Asha Mwakyonde
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM), kinatoa huduma ya ushauri wa kisheria hasa katika mikataba ya biashara ambayo wengi wamekuwa wakidhulumiwa kutokana na kutojua sheria vizuri katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, ‘Saba Saba’.
Hayo yamesemwa leo Juni 30,2025 jijini Dar es Salaam katika maonesho hayo na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko UDOM, Rose Joseph, amesema kuna watu wanaingia mikataba na wanapata changamoto kwa kutokujua utaratibu mzuri wa kuingia katika mikataba hiyo hususani wageni.
"Chuo kinatoa huduma ya msaada wa kisheria bure katika kipindi hiki Cha maonesho ya Saba Saba na hata wale ambao wanakesi ngumu za kwenda kusimamia mahakamani chuo kipo tayari kupitia wataalam wake katika kipindi hiki,"amesema Mkurugenzi huyo.
Ameeleza kuwa kuwa ni nafasi nzuri kwa chuo hicho kushiriki katika maonesho hayo kwa kuwa wanakutana na wadau wao mbalimbali ambao ni wanataaluma pamoja na kuzitangaza shughuli zinazofanywa na chuo hasa bunifu kupitia zinafanywa na wanafunzi.
Mbalimbali na masuala ya sheria mkurugenzi huyo ameeleza katika maonesho hayo chuo hicho
kina wataalam wanaotoa ushauri namna ya ulaji sahihi kwa lengo la kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.
Amesema ulaji sahihi utamuongoza mtu kula vyakula vyenye afya na kuweza kupunguza magonjwa yasiyoambukiz yakiwamo presha, sukari na mengine ambayo yanekuwa ndio tatizo kubwa kwa Watanzania.
Ameongeza kuwa chuo hicho kimebobea katika masuala ya lishe na kwamba kina wataalamu wanaoweza kushauri tiba lishe ambayo anaweza kutumia mtu yoyote ili kuwa salama.
0 Comments