TASAC: SEKTA YA BAHARI INA FURSA NYINGI ZA KIUCHUMI

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC),Mohamed Salum amesema amesema sekta ya bahari ina fursa nyingi ambazo wananchi wamekuwa hawazifahamu ikiwemo maeneo ambayo wanaweza kusoma na kupata ajira kwa urahisi zaidi na kwamba inaongoza kwa mchango mkubwa kiuchumi hasa katika shughuli za usafirishaji.

Hayo ameyasema leo Julai 7, 20225 katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, ‘Saba Saba' alipotembelea banda la TASAC amesema nchi ina upungufu mkubwa wa wataalamu kupitia sekta hiyo na kwamba zipo ajira na fursa mbalimbali.

Ameongeza kuwa duniani kote kuna upungufu wa mabaharia kwa mujibu wa takwimu za uhitaji mabaharia hawajawahi kutosha kwenye Meli.

Aliwataka wananchi kutembelea banda la TASAC kwa lengo kufahamu sekta ya bandari na mchango wake katika uchumi katika nchi.

TASAC ina majukumu mbalimbali ikiwemo majukum Udhibiti wa usafiri majini pamoja na kuchagiza sekta usafiri nchini.

Post a Comment

0 Comments

TPDC YAIBUKA MSHINDI KWA KULINDA MAZINGIRA