BRELA YAPATA TUZO KUNDI BORA LA UWEZESHAJI BIASHARA NA UWEKEZAJI SABA SABA 2025

Na Asha Mwakyonde, DAR

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),umepata tuzo ya ushindi katika kundi bora la Uwezeshaji Biashara na Uwekezaji ambapo imeendelea kutoa huduma kwa kutumia Mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao ORS ambao

umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza urasimu, kuongeza ufanisi na kuwezesha wananchi wengi zaidi kuanzisha biashara kwa urahisi na haraka.

BRELA imeshinda tuzo hiyo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Sabasaba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 7,2025 mara baada ya kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Meneja wa Sehemu ya Alama za Biashara na Huduma Seka Kasera, ameeleza kuwa ushindi huo ni ushahidi tosha wa jitihada kubwa zinazofanywa na BRELA ikiwa kuboresha huduma, kukuza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara, na kuendana na kasi ya mapinduzi ya kidijitali kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa taifa.

Kasera amesema kuwa katika kipindi chote cha maonesho hayo Wakala huo ilitoa huduma za papo kwa papo zinazopatikana kwa njia ya mtandao, jambo lililowavutia wadau mbalimbali.

Amefafanua kuwa tuzo hiyo haimaanishi tu heshima bali ni mwito kwa wadau mbalimbali kutumia huduma za BRELA katika kurasimisha biashara zao.

Kasera aliwapongeza kwa watumishi wote wa BRELA kutokana na juhudi na weledi waliouonesha wakati wote wa maandalizi wa maonesho hayo pamoja na ushiriki wao.

"Mshikamano na umoja kati ya BRELA na wadau ndio msingi wa mafanikio tunayoyaona leo kuwa wao ndio chachu ya mafanikio ya taasisi hiyo," ameeleza.

Kasera ametoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali wa BRELA ambao wameendelea kutumia mifumo ya mtandao kusajili biashara, kampuni, alama za biashara na kupata leseni, "amesema.

Amesema kuwa wataendelea kuwahudumia wananchi, wateja hata nje ya sabasaba huku akiwatoa hofu wateja wao kwamba huduma zinaendelea katika ofisi zao zote.

Amewataka wananchi kuendelea kufika, kutembelea kwenye banda la wakala huo katika maonesho hayo kwa lengo la kupata elimu na kuweza kusajili majina ya Biashara zao, kupata alama za biashara huku akisema usajili unafanyika wa papo kwa hapo.

Post a Comment

0 Comments

PURA YAIPONGEZA SERIKALI AGENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA