TANESCO YATOA ZAWADI YA MAJIKO SABA SABA KUHAMASISHA NISHATI SAFI


Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam 

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO),imetoa zawadi ya majiko ya umeme kwa Wananchi waliofika katika banda la Shirika hilo lililopo kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa 'Saba Saba' lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi hao wanatumia Nishati safi ya kupikia.

Hayo yamesemwa leo Julai 7,2025 jijini hapa na Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Umeme Tanzania wa Shirika hilo Lazaro Twange ambapo amewahakikishia watanzania kuendelea kuwapatia elimu juu ya matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia.

Ameongeza kuwa wananchi waliofika katika banda hilo wamepata fursa ya kupata elimu ya nishati safi ya kupikia pamoja na kupatiwa majiko.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wanatekeleza maelekezo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwamba watanzania wahame kwenye kutumia nishati isiyokuwa safi na kutumia iliyosafi.

"Tuna majiko haya ya umeme yamefanyiwa utafiti na kuthibitika kuwa unaweza kupikia na chakula kikaiva kwa kutumia chini ya Unit moja tu," amesema Mkurugenzi huyo.

Naye Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO), Sadock Mugendi amesema

hivi karibuni wamemaliza mradi wa kusafirisha umeme kutoka Tabora mjini kuelekea Katavi wenye kilomita 383 na una msongo wa Kilovolt 132.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakisambaza na kusafirisha umeme maeneo mbalimbali vijijini.

Post a Comment

0 Comments

TPDC YAIBUKA MSHINDI KWA KULINDA MAZINGIRA