TEA YAPIGIA DEBE FURSA ZA WADAU KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU

Na Asha Mwakyonde,Dar es Salaam 

MAMALAKA ya Elimu Tanzania (TEA), inawaomba wadau mbalimbali wa maendeleo ya elimu kuchangia Mfuko wa elimu wa Taifa ili uendelee kutekeleza majukumu ya kujenga miundombinu ya elimu hasa pembezoni mwa Miji ambapo ambapo mamalaka hiyo imejikita.

Hayo yalisemwa leo Julai 4,2025 jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, ‘Saba Saba' na Kaimu Meneja wa Utafutaji Rasilimali na Hamasa kutoka Mamalaka hiyo, Dk. George Mafulu ameeleza kuwa TEA ipo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambayo ina jukumu kubwa la kusimamia mfuko wa elimu wa Taifa.

Amesema mfuko huo umeundwa kisheria chini ya Sheria Namba 8 ya mwaka 2001 ukiwa na majukumu ya kutafuta rasilimali fedha na vifaa kwa ajili ya kugharamia shughuli za elimu.

Kaimu Meneja huyo amezitaja baadhi ya shughuli kubwa zinazogharamiwa na mfuko huo kuwa ni pamoja na miundombinu ya shule kuanzia ngazi ya elimu ya shule msingi hadi Chuo kwa Tanzania Bara huku akisema kwa upande wa Zanzibar wanagharamia miradi ya elimu katika ngazi ya Chuo KiKuu.

Dk. Mafulu amefafanua kuwa wanakusanya rasilimali kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo wadau wa elimu.

Amefafanua kuwa kuna faida nyingi za wadau kuchangia katika mfuko huo ikiwa ni pamoja na kupata hati ya utambulisho kwa wadau ambao wanachangia mfuko wa elimu ambayo ina sainiwa na mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa TEA na Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

" Wachangiaji wanaweza wakapata unafuu wa kulipa kodi wakipata cheti hiki cha utambulisho, pia mchangiaji anapata nafasi ya kutangazwa kama mdau muhimu wa maendeleo katika majukwaa mbalimbali ambayo tunafanya shughuli zetu na anaingia katika hifadhidata, 'database' yetu ya kudumu amesema.

Ameeleza kuwa database hiyo inafika kwa mamalaka mbalimbali na kwamba hadi kwa Rais kuona ni wadau gani wamemsaidia katika kuendeleza sekta ya elimu huku akisema hayo ndio majukumu yanayofanywa na mfuko wa elimu wa Taifa.

Dk. Mafulu amesema TEA inasimamia mfuko wa puendelezaji wa ujuzi 'Skills Development Fund (SDF)', ambao umelenga zaidi katika kuwapa wanufaika mbalimbali ujuzi huo na kuuendeleza ujuzi walio nao.

"Walengwa wa mfuko huu wanatoka katika maeneo tofauti tofauti wanaweza wakawa ni wale waomaliza elimu rasmi na wale ambao hawajapata fursa ya kupata elimu rasmi hivyo wote wanapata nafasi ya kujifunza na kuendeleza ujuzi walizonazo zinazoenda kulenga kusaidia katika uzalishaji amesema.

Ameeleza kuwa ushiriki wa TEA katika maonesho hayo kwa kiasi kikubwa wanataka kuonesha wananchi shughuli ambazo wanazifanya na kutoa fursa kwa watu kujifunza, kujua ni miradi gani wanaifanya na wanaweza kushiriki vipi miradi ambayo mamalaka hiyo ina ifanya.

Kwa upande wake mwananchi aliyetembelea banda TEA, Mwalimu wa shule ya sekondari Gotfrid Gabriel kutoka Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera ameipongeza mamalaka hiyo kwa kujikita katika kujenga miundombinu kwa shule zilizopo pembeni mwa Miji.

Ameongeza kuwa Shule nyingi alizozitembelea katika Mkoa wa Kagera hazina majengo ya Utawala huku akisema walimu wengi wanafanyia kazi zao katika madarasa kama ofisi.

"Mmejielekeza katika mazingira ambayo hayafikiki mmneweza kujenga maabara, nyumba za walimu pamoja na ofisi ambapo walimu walikuwa wanatumia madara kama ofisi," amesema.

Aidha Mwalimu huyo amesema kuwa katika shule yake wana tatizo la nyumba za walimu huku akiomba mamalaka hiyo kwasaidia.


Post a Comment

0 Comments

TEA YAPIGIA DEBE FURSA ZA WADAU KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU