Na mwandishi wetu,Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, ameeleza kuwa uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika taasisi za umma ambapo Ofisi ya Msajili wa Hazina imewezesha kuimarika kwa fedha katika mashirika ya umma yaliyokuwa na mitaji hasi.
Hayo ameyasema leo Julai 4, 2025, alipotembelea banda namba 39 (Ukumbi wa Kilimanjaro),katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam 2025, ‘Saba Saba' amesema taasisi na mashirika ya Umma yaliyokuwa yanapata hasara mfululizo, ambapo sasa yameweza kuondokana na utegemezi wa ruzuku ya Serikali na kufanikiwa kutoa gawio.
Kikwete aliyataja baadhi orodha ya mashirika ambayo kwa sasa yanajiendesha kwa ufanisi ni pamoja na Shirika la Taifa la Madini (STAMICO), Shirika la Umeme (TANESCO), na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Alisema baadhi ya mashirika hayo ni pamoja na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ambapo mchango wake katika Mfuko Mkuu wa Serikali ulikuwa Sh10.5 bilioni katika mwaka wa fedha 2024/25.
Aidha ameipongeza Ofisi ya Msajili kwa mageuzi makubwa iliyofanya katika mashirika ya umma hukub
akiishukuru Ofisi hiyo ya Hazina chini ya uongozi imara wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, kwa kuwezesha taasisi za umma kuongeza ufanisi wao.
Waziri huyo alieleza kuwa serikali itaendelea kuiunga mkono ofisi ya Msajili wa Hazina katika kuhakikisha safari ya mageuzi inafanikiwa.
“Mmekuwa mkifanya kazi kwa bidii hivyo endeleeni kufanya hivi, kama kuna mambo mnataka yabadilike katika taasisi ambazo ziko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hesabuni mmepata ushirikiano kutoka kwetu,” alisema Kikwete.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Ofisi hiyo Sabato Kosuri, alisema kwa mwaka huu wa fedha uliopita, pamoja na kuongeza mchango kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kutoka Sh155.7 bilioni mwaka 2023/2024 hadi Sh181 bilioni mwaka 2024/2025.
Alifafanua kuwa matumizi ya kawaida kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa bandari pia yamepungua kwa kiasi cha Sh505.59 bilioni sawa na ufanisi wa asilimia 46.
"Kumekuwa na ongezeko kubwa la ufanisi kwenye baadhi ya Mashirika kutokana na mageuzi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika katika Mashirika ya umma," alieleza.
Alisema ufanisi umeimarika kwa kiasi kikubwa ambao unaonekana kwenye Mamlaka ya Bandari.
0 Comments