MYUMBILWA ATOA WITO KWA WATANZANIA KUTUMIA TAFITI ZA GST KATIKA SHUGHULI ZA MADINI,KILIMO, NA UJENZI

Na Mwandishi wetu, DODOMA 

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania GST Bi. Yokbeth Myumbilwa ametoa wito kwa Watanzania kutumia Tafiti zinazofanywa na Taasisi hiyo katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta Madini, Kilimo, Maji na Ujenzi.

Mwenyekiti wa Bodi Bi. Myumbilwa ametoa Rai hiyo Jijini Dodoma alipotembelea Banda la GST katika kilele cha Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane nane ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya John Malecela Jijini Dodoma ambapo amewataka watanzania kutumia tafiti za GST katika shughuli mbalimbali ikiwemo za Uchimbaji Madini, Kilimo na Ujenzi.

Aidha, amesisitiza watanzania kuweza kupata machapisho mbalimbali ya GST ikiwemo chapisho la Madini Yapatikanayo Tanzania na chapisho la Madini Viwanda ambayo yanaonesha aina za madini yanayopatika katika Mikoa yote ya Tanzania.

‘’Nawasihi watanzania wafike katika ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania GST ili waweze kupata machapisho haya ambayo yanataarifa nyingi za madinini yanayopatikana kuanzia ngazi ya kijiji, Wilaya hadi Mkoa,” amesema Myumbilwa.

Sambamba na hayo, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya Jirani kutembelea banda la GST ili kuona na kupata taarifa mbalimbali zinazohusu Madini ya Kilimo hapa nchini.

“Naomba nitumie nafasi hii kuwakaribisha watanzania na wale wote ambao mmejitokeza kuja katika viwanja vya Nanenane wafike katika banda la GST ili waweze kupata taarifa mbalimbali zinazohusu Madini Kilimo ambayo yanatumika kutengeneza mbolea,” amesema Myumbilwa.

Katika hatua nyingine, ameipongezal Taasisi ya GST kwa kuandaa ramani inayoonesha Madini mbalimbali ambayo yanatumika kurekebisha udongo katika maeneo yenye upungufu wa Madini fulani na kuongeza kuwa ramani hiyo itawasaidia sana wakulima kurutubisha udongo katika maeneo ya Kilimo.






Post a Comment

0 Comments

Mgomba wa Chama cha National League for Democracy (NLD),Doyo Hassan Doyo akiingia na usafiri wa bajaji  MC 816 CNUkuchukua fomu ya urais 2025.