Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WANAFUNZI kutoka Chuo cha Mipango ya Maendeleo ya Vijijini (IRDP), jijini Dodoma wametembelea banda la Heifer International Tanzania katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane, na kujifunza fursa mbalimbali za kujiajiri kupitia mnyororo wa thamani wa maziwa.
Kupitia mjadala uliofanyika wakati wa ziara hiyo, wanafunzi walihamasika kuhusu nafasi ya vijana katika mageuzi ya kilimo nchini kupitia ubunifu, ujasiriamali na matumizi ya teknolojia.
Wanafunzi hao walionesha kuvutiwa na mikakati inayotekelezwa na Heifer, hususan utoaji wa mafunzo, usaidizi wa kitaalamu kwa wafugaji na uhusiano wa kibiashara unaowawezesha vijana kufikia masoko.
Programu kama AYuTe Africa Challenge zilitajwa kuwa miongoni mwa nyenzo muhimu zinazowasaidia vijana wabunifu kupata majukwaa, zana na uwekezaji kwa ajili ya kukuza suluhisho za kiteknolojia katika kilimo, hasa kwenye mifumo ya chakula.
Heifer International Tanzania imeendelea kujitolea kuwa sehemu ya mabadiliko chanya kwa kuwawezesha vijana kuwa mawakala wa maendeleo katika sekta ya mifugo, kwa lengo la kujenga mustakabali endelevu na wenye usawa zaidi.
#HeiferTanzania #Nanenane2025 #VijanaNaKilimo #MnyororoWaMaziwa #AYuTeAfrica #KilimoNaTeknolojia #KujiajiriKupitiaMifugo #KilimoJumuishi #MaishaYanabadilika
0 Comments