Septemba 26, 2026 | Loliondo, Arusha
WANAWAKE, wajane na wazee katika Wilaya ya Ngorongoro, Mkoa wa Arusha, wanatarajiwa kupata fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili katika maisha na shughuli zao za kiuchumi, wakati Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mhandisi Maryprisca Mahundi, akianza ziara ya kikazi wilayani humo.
Mahundi amewasili katika Tarafa ya Loliondo, ambako amepokelewa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hamza Hamza, na anatarajiwa kukutana na vikundi mbalimbali vya wanawake, wakiwemo wajane, pamoja na makundi ya wazee.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri atatembelea pia vikundi vya Tupendane Loliondo na Naretu Sukenya kwa ajili ya kujionea shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanachama wake na kusikiliza changamoto zinazohitaji ufumbuzi.






0 Comments