NA ASHA MWAKYONDE,MBEYA
NAIBU Waziri wa Kilimo Antony Mavunde amesema kuwa Sh. Bilioni 27 zitatumika kujenga maghala katika maeneo ya uzalishaji huku akisema lazima wataangalia namna ya kumkopesha mkulima kwa riba nafuu.
Hayo ameyasema jijini Mbeya juzi katika Kongamano la shamba darasa amesema Katika hatua ya kuwakopesha wakulima benki zitaangalia ili ziweze kuwawezesha wakulima hao waweza kuzalisha Mazao, chakula kwa wingi.
Mavunde ameongeza kuwa serikali ina changamoto mafuta ya kula ambapo inatumia milioni 74 kuingiza mafuta hayo na uhitaji ni tani 650,000 wakati nchi inazalisha tani 250,000 hadi 300,000.
" Tunakaribisha wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza tuondokane na kilimo cha ekari moja moja na twende tukawekeza kwenye mashamba makubwa, amesema Naibu Waziri huyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI),Dk.Goeffrey Mkamilo amesema kuwa wana aina ya mbegu 380 katika mazao mbalimbali na kwamba ifikapo Juni 30, 2023, watakuwa wamefikia aina za mbegu 400.
Amesema kwa kutumia mbegu bora zenye ukinzani na magonjwa ambazo zimehakikiwa na Wizara tija inaongezeka kutoka tani 10, 25 hadi 70.
Mkurugenzi huyo amesema wanatarajia kuzalisha tani 1400 za mbegu ambazo ni za daraja la awali la msingi ifikapo Juni 30, 2023.
Amesema lengo la kuzalisha mbegu hizo ni kuwapatia Wakala wa mbegu za kilimo (ASA),ili kuziihaki na kuwafikishia wakulima.
Dk. Mkamilo ameongeza kuwa TARI ina mkakati wa kuzalisha miche milioni 50 ifikapo Juni 30 2023.
Awali Mshauri wa Sera za Kilimo Profesa David Nyange amesema kuna vitu vitatu ili kufikia malengo yenye tija kuwa na mbegu bora, miundombinu bora za Nishati na lishe kwenye mazao ambayo ni afya ya udongo.
Naye Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS), Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),Daniel Masolwa amesema sera na mipango ya serikali ipo wazi mwaka Agosti 23 mwaka Kuna zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Amesema wanakusanya takwimu za kilimo kwa kuwa zina umuhimu mkubwa katika mstabali wa nchi.
"Tukiwa na takwimu nzuri za kilimo ni rahisi kujenga hoja agenda ya 10/30 na tukizalisha zaidi mazao yatauzwa nje ya nchi na kupata fedha za kigeni," amesema.
0 Comments