JKT YAJIPANGA KUKABILIANA NA UHABA WA MAFUTA YA KULA


 NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA

MKUU wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema wana mikakati yao ni kuhakikisha wanapambana na uhaba wa mafuta ya kula nchini huku akisema , JKT limejipanga kukabiliana na hali hiyo na  tayari wameshaanza kuboresha shamba la michikichi Kikosi 821 Kigoma.

Akizungumza Jijini Mbeya katika wakati akimwakilisha Mkuu wa JKT katika maonyesho ya Nane Nane kwenye viwanja vya John mwakangale Jijini Mbeya, Brigedia Jenerali Mabena amesema kwa sasa wanalima michikichi na kwamba watahakikisha wanapanda ekari 2,000 za michikichi.

Brigedia Jenerali Mabene ameongeza kuwa mwelekeo wao ni kuhakikisha  shamba hilo na kupata  mafuta kutokana na michikichi.

Brigedia Jenerali amesema,JKT wanataka kuondoakana na kilimo cha kutegemea mvua,ambapo Jeshi hilo limekuja na kilimo mkakati wa umwagiliaji ambapo tumeanza kikosi 837 Chita tayari Skimu ya umwagiliaji imeshafikia zaidi ya asilimia 80 ya ekari 2500.

" Mpango uliopo ni kulima ekari 12,000 zilizopo kikosi cha Chita zote zinajengewa skimu ya umwagiliaji na hivyo JKT kuondokana na kutegemea mvua kwani tutakuwa na uhakika na tunachokilima na uhakika wa nini tunataka kuvuna," ameeleza.

Akizungumzia mafanikio ya Jeshi hilo siri ya mafanikio yao katika uzalishaji wa mazao ya mashamba ya JKT ni mawasiliano yanayofanywa na Jeshi hilo kujua hali ya hewa ya kipindi husika.

Brigedia Jenerali Mabena amesema,wamekuwa wakiwasiliana na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kujua hali ya mvua ya kipindi husika na kutaka kufahamu gani wanaweza kuanza shughuli ya kupanda mazao.

Amesema,hatua hiyo imefanya pamoja na mabadiliko ya tabianchi lakini bado katika vipando vya JKT na mashamba yake kwa ujumla yaliyopo vikosini kuendelea  kufanya vizuri mazao yameweza kustawi kwa jinsi ambavyo walikuwa wametarajia.

“Siri ya mafanikio kwa JKT katika uzalishaji wa mazao katika mashamba yake ni kwamba sisi tulishaiona hiyo changamoto ya mabadiliko ya tabianchi,kwa hiyo tunachokifanya ni kuwasiliana na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kujua hali ya mabadiliko ya tabianchi hasa kwenye eneo la mvua,

“Kwa hiyo walikuwa wakituambia msimu huu mvua zitawahi au zitachelewa na hata kama zitawahi basi zitakuja kwa kiwango kidogo sana kwa hiyo baada ya kupata taarifa hiyo JKT tulikaa chini na kuweza kuona kwamba ni aina gani ya mbegu ambazo zitaendana na hali ya hewa iliyopo,lakini pia tuanze kulima mapema”amesema na kuongeza kuwa

“Mfano kikosi cha 847 Milundikwa,pale kikosini wamefanikiwa sana ,wameweza kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa sababu baada ya kuwasiliaana na mamlaka ya hali ya Hewa waliweza kulima mapema na kupanda mapenda na kutumia mbegu zenye uwezo wa kuhimili ukame.

Post a Comment

0 Comments

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA MIFUMO THABITI YA NISHATI JADIDIFU KUKIDHI MAHITAJI YA NISHATI