TBA KUHAKIKISHA WATUMISHI WA UMMA WANAPATA MAKAZI BORA


 Mtendaji Mkuu wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Daud Kandoro akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda lao.

NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA),umetekeleza ujenzi wa nyumba 3,500 na ujenzi wa nyumba 150 ukiwa unaendelea jijini Dodoma na kwamba lengo la ujenzi huo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanapata makazi bora yatakayowafanya waongeze tija katika kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza Jijini Mbeya  alipotembelea banda la TBA katika maonyesho ya Wakulima Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya yanakofanyika Kitaifa Mtendaji Mkuu wa TBA, Msanifu Majengo Daud Kandoro amesema wanatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya afya katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini .

"Nchini kuna miradi tunatekeleza katika mikoa minane ikiwemo ya ujenzi wa vihenge katika utunzaji wa nafaka,pia tuna miradi ya Afya katika wilaya ya Tunduma,Kyela kupitia mradi wetu wa Buni Jenga.”amesema Kandoro

Katika hatua nyingine amesema,pamoja na kujenga lakini TBA pia ni wabunifu wa majengo huku akisema,ujenzi wa awamu ya pili ya mji wa Serikali mkoani Dodoma ubunifu Aidha amesema,hivi sasa wanasimamia miradi 15 ya majengo na wanajenga Ofisi Rais Utumishi katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu huyo amesema,katika kuhakikisha kazi zao zinakuwa na ubora,wanatumia vifaa na mitambo ya kisasa kama vile mitambo ya kuchakata zege uchimbaji na vifaa vingine vinavyotumika katika ujenzi.




Post a Comment

0 Comments

GEITA YAUPOKEA MRADI WA BILIONI 17 KWA AJILI YA KUSAMBAZA UMEME KWENYE VITONGOJI 105