Rais Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa ujenzi wa kituo cha pamoja cha forodha Kasumulu wilayani Kyela katika mpaka wa Tanzania na Malawi Agosti 7, 2022. Mradi huu unajengwa na Kampuni ya China Geo-Engineering Corporation (CGC) na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Engineering Consultant Group (ECG) kutoka Misri.
Mtendaji Mkuu wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Daud Kandoro akitoa maelezo mafupi kuhusu mradi wa ujenzi wa kituo cha Forodha mpakani mwa Tanzania na Malawi.
NA ASHA MWAKYONDE,MBEYA
RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi Kuulinda na kuutunza pampja na kutoa ushirikiano wa watakao haribu miundombinu mradi wa kituo cha Forodha Kasumuku, Wilayani Kyela katika mpaka wa Tanzania na Malawi.
Hayo ameyasema Agosti 7, 2022, wakati akiweka jiwe la msingi kwenye mradi huo unaojengwa na Kampuni ya China Geo-Engineering Corporation (CGC) na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Engineering Consultant Group (ECG) kutoka Misri.
Rais Samia amesema wananchi hao wakiitunza vizri mradi huo utakuwa endelevu kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Ametoa pongezi kwa waliojenga mradi huo huku akisema ni matumaini yake kwamba atarudi kwa ajili ya kuuzindua ili uanze kuhudumia wananchi .
" Mradi huu ni wakwenu hivyo lindeni miundombinu yake ili ukae kwa kipindi kirefu na kufanya hivyo utaweza kuchangia Pato laTaifa letu," ameeleza.
0 Comments