NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI), imekipatia chuo Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ukarabari wa majengo, ili kiweze kudahili wanachuo wengi zaidi ambapo kwa sasa wapo 400.
Akizungimza katika maonesho ya wakulima na wafugaji maarufu nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale ambapo kitaifa yanafanyika mkoani hapa, Robert Shilingi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha kupitia ukarabari huo wanaweza kudahili Wanafunzi 800 hadi 1000 baada ya kuboresha.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo ya fani za uashi na useremala,fani ya uundaji wa vyuma, ubunifu wa mitindo na Ushonaji wa Mavazi, upishi na Usimamizi wa hoteli, udereva, ufundi magari, ujasiriamali stadi za maisha, fundi bomba, uungaji na usambazaji wa vimiminika, fani ya umeme majumbani, kilimo na Ufugaji.
Amesema wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanafundishwa kwa vitendo na anaweza kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Ameongeza wameanza kulima mafuta ya alizeti kupitia wanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha na sekondari.
Ameeleza kuwa kwa Sasa wataanza kuchaka wenyewe kutokana na wanafunzi hao kutengeneza mashine ya kuchakata mafuta ya alizeti.
"Shirika la Elimu Kibaha ni Taasisi ya Umma iliyochini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),lilianzishwa kwa tangazo la serikali namba 2 la mwaka 1970, chini ya sheria ya mashirika ya Umma namba 2057 na marejeo ya 2002," amesema.
Amesema kuwa Shirika hilo lina majukumu Saba ni utoaji wa Elimu, mafunzo dhidi ya maadui watatu wa maendeleo ambayo ni maradhi, ujinga na umasikini.
0 Comments