FCS YATOA RUZUKU YA BILIONI NNE KWA ASASI ZA KIRAIA 89


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS),Francis Kiwanga,akisisitiza jambo kwa washir8iki wa warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI  89 zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.

Baadhi ya a washiriki wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS),Francis Kiwanga,(hayupo pichani) wakati wa warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI 89 zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.

NA ASHA MWAKYONDE,DODOMA 

ASASI za Kiraia (AZAKI),89 Tanzania Bara na Visiwani  zimepatiwa Sh.Bilioni nne na Shirika la Foundation for Civil Society (FCS), kwa lengo la kutekeleza miradi ya kimaendeleo chini ya program ya utawala bora katika sekta za  elimu, maji, kilimo na afya.

Akizungumza  leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga,wakati wa  warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI hizo amesema wamepata wadau 89 wa MIKOA yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kati ya 1,200 zilizoomba.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa lengo ni kusukuma agenda ya utawala bora huku akisema  FCS imejikita katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha yao.

Akizungumzia  eneo  jingine la utawala bora amesema  ni vita dhidi ya kuondoa ukatili wa kijinsia  na kwamba  kundi la vijana kuhakikisha rasilimali zinazotolewa na serikali na wadau wengine pamoja na makundi hayo na watu wenye mahitaji maalum.

Pia katika sekta za  elimu, afya na kilimo, usawa wa kijinsia, ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.

Ameongeza kuwa FCS imepitisha mpango mkakati mpya wa mwaka 2022-2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanaopata haki za kiuchumi, kijamii na kuboresha ubora wa maisha yao.

Kiwanga amesema  kuwa kumekuwepo ongezeko la migogoro katika rasilimali hivyo kwa sasa kuna taasisi 10 zitafanya kazi ya kuitatua hususani maeneo ya Kusini, Morogoro na Kilosa.

Amesema FCS imeweka mfumo madhubuti wa kuhakikisha  kila shilingi inatumika kwa lengo lilokusudiwa huku  taasisi zizofuata utaratibu watachukua hatua kali.       

Kwa upande wake ,Meneja Programu Utawala Bora FCS, Edna Chilimo amesema  FCS wanafanya kazi na mashirikia madogo  ambao ni wabia na viongozi wa klasta za programu wambao wanafanya kazi katika ngazi ya taifa.

Amesema wanafanya kazi na asasi za kijiji, kata na wilayani huku wabia ni mashirika tunayofadhili ni wadau muhimu.

Chilimo amesema  mashirika yanayofadhiliwa na FCS sio waruzukiwa tu, ni wabia pia na kwamba baadhi ya misingi ya ubia ni uelewa wa pamoja,malengo ya pamoja, na kuaminiana ili kuweza kufikia malengo ya pamoja.

“Tumekuwa walezi wa sekta ya AZAKI, tumechangia ukuaji wa sekta, miaka ya nyuma tulitoa fedha kwa Azaki kujisajili na sasa kuna Azaki zimekua, kutoka shirika dogo hadi kuwa mashirika makubwa yenye sifa,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la TAWSEI kutoka Mkoa wa Tanga, Bernadethe Choma,amesema wao kama NGO’S kupitia ruzuku wanazopewa zitaenda kuboresha maisha ya wakazi wa maeneo husika.


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU