RAIS SAMIA AWATAKA WANANCHI WA MBEYA KUKITUMIA CHUO CHA VETA


 NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA

WANANCHI wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wametakiwa kukitumia chuo cha Ufundi Stadi kinachomilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ili kiwasaidie kupata stadi zitazowawezesha kujiajiri wenyewe na kujikwamua kiuchumi na  kuchangia pato la Taifa.

Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibu mkoni Mbeya wakati akiwahutubia wananchi wa Mbarali mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa chuo cha VETA wilayani humo,Rais Samia amesema,serikali imeamua kujenga vyuo hivyo  katika kila wilaya na maeneno mbalimbali Tanzania.

“Vijana wa Mbarali ndiyo takaosoma hapa,hatutaki watu wa maeneo mengine waje wasome hapa na mtafundishwa kazi zenu zinazowazunguka hapa,kwa hiyo leo tumekuja kuweka jiwe la msingi ,chuo kimekamilika bado kumalizia mambo madogo madogo .”amesema Rais Samia.                                                        

Ameongeza kuwa ,matarajio ya Serikali ni kuhakikisha mwisho wa mwaka huu chuo hicho kinaanza kuchukua wanafunzi wa kusoma na kuondoka(wanafunzi wa kutwa) kuanzia mwakani chuo hicho kitaanza kuchukua wanafunzi wa bweni kwa lengo la kuwapa vijana elimu na ujuzi ili wakajiajiri na kujipatia kipato kitakachowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi  kujitokeza kwa wingi kushuhudia uwekaji jiwe hilo katika  chuo hicho ambacho kinamaslahi mapana kwa wananchi hao na Taifa kwa ujumla.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Antony Mzee amesema chuo hicho kimejengwa kina  hadhi ya wilaya,huku akitoa rai kwa wananchi hao kutumia fursa hiyo vizuri.

"Fursa hii ya mafunzo ya VETA ni nzuri  na serikali imethamini sana eneo hili na imoena kuna jambo muhimu sana ambalo wananchi wa Mbarali wanatakiwa kupata ujuzi.”amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.




 


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU