VIJANA WAHAMASISHWA KUINGIA KATIKA KILIMO CHA MKONGE


NA ASHA MWAKYONDE,MBEYA

MWENEYKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge Nchini (TSB) Mariam Nkumbi anaihamasisha jamii hasa vijana kujikita katika kilimo cha mkonge kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla kwa kuwa uwekezaji ni mzuri.

Pia Nkumbi ameeleza kuwa zao la mkonge uwekezaji wake unafaida kwani hurisishana.

Akziungumza kwenye maonyesho ya Nane Nane Jijini Mbeya uwekezaji wake mkulima akipanda zao la mkonge na akianza kuvuna atavuna kwa muda wa mika 15.

Mwenyekiti huyo amesema amewashauri vijana kujikita katika kilimo cha mkonge na kuanacha na ururulaji ambao utawaletea matatizo baadae kama kujiingiza kwenye makundi yasiofaa.

“Njia pekee ya kuwawezesha na kuwainua wananchi hususan vijana kiuchumi,ukipata eneo lako la zao mkonge ukawekeza katika kipindi cha miaka 15 wewe utakuwa unavuna tu.”ameongeza.

“Benki nyingi zinatoa mikopo ambapo mkonge ni zao mojawawapo ambalo benki inaliangalia katika kutoa mikopo kwa vijana hasa kwenye kilimo ambayo imeshushwa riba,”amesema.

Ameongeza kuwa zao la mkonge linastawi katika mikoa 16 hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa maendeleo ya zao la Mkonge,Bodi ya Mkonge Tanzania Olivo Mtung'e amesema lengo la Bodi ya Mkonge ni kuongeza matumizi ya mmea wa mkonge tofauti na sasa ambapo bado tunategemea matumizi ya bidhaa ambazo ni kama asilimia mbili tu.

Amesema,wanahitaji kuongeza matumizi ya zao hilo hadi kufikia asilimia 50 kutoka na zao hilo kuwa na masoko makubwa ya mahitaji ya zao hilo ndani nan je ya nchi.



Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU