RAIS SAMIA AIPONGEZA TBA UJENZI WA OFISI YA RC MBEYA

Rais Samia Suluhu Hassan akizindua jenga la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lililojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).


Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Jenga la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lililowekwa jiwe la msingi na Rais Samia Suluhu Hassan.



NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA


RAIS Samia Suluhu Hassan amesema ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lililojengwa na Wakala wa majengo Tanzania (TBA), limejengwa vizuri kwa kiwango ingawa gharama yake ni Sh. Bilioni 6.

Akizungimza wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika jengo hilo jijini Mbeya juzi Rais Samia amesema jengo hilo limetumia Sh bilioni 6, na wataaendelea kujenga ya aina hiyo katika kila mikoa ya makao makuu ya Kanda.

Rais Samia ameongeza kuwa ujenzi wa jengo hilo ameridhika nao huku akiwapa pongezi wanambeya kwa kuwa fedha iliyotumika katika ujenzi huo imeendana na uhalisia halisi. 

"Nilirushiwa picha ya jengo ninaloenda kulizindua nilifurahishwa kwa kuona jengo limejengwa vizuri na kwa uhimara zaidi. Tunaendelea kujengo majengo yaliyobora, tumeanza pia kuboresha majengo ya mahakama zetu," amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kandoro amesema ni wajibu wao kujenga majengo bora ya serikali na kwa gharama nafuu huku akimshukuru Rais Samia kwa kuweka jiwe la msingi katika jengo hilo.

Arch. Kandoro amefafanua kuwa ubunifu katika jengo hilo umeanzia kwenye ofisi za TBA pamoja na mji wa Serikali Dodoma ulipo Mtumba huku akisisitiza kuwa wapo tayari pale wanapohitaka kujenga majengo kwani ndio shughuli zao.



Post a Comment

0 Comments

WAZIRI SILAA AZINDUA MNARA WA MAWASILIANO KATA YA MAKURU, SINGIDA