WAKULIMA WASHAURIWA KUTEMBELEA BANDA LA MOI

 Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka  Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Dk. Sharifu Luena akiwaelezea watu waliotembelea banda lao kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo.

NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA

TAASISI ya Mifupa na Tiba Muhimbili (MOI), imesema ili kuingia kwenye kilimo cha biashara wanahitajika watu wenye afya bora hivyo wakulima wametakiwa kutembelea banda la taasisi hiyo ili kupata ushauri pamoja elimu.

Pia taasisi hiyo imewaomba Watanzania kuwa tayari kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotajariwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu ili serikali iweze kupata takwimu sahihi kwa ajili ya kuweka mipango bora ya maendeleo ikiwamo ya kilimo na afya kwa ujumla.

Akizungimza katika maonesho ya wakulima na wafugaji maarufu nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale ambapo kitaifa yanafanyika mkoani hapa Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka MOI, Dk. Sharifu Luena amesema lengo la kushiriki maonesho hayo ni kuonesha jitihada za makusudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.

Dk. Luena amesema kuwa huduma amabazo wanazitoa katika maonesho hayo ni ushauri wa shida zote za mifupa, Ubongo, Uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu.

Ameeleza kuwa wanajua watu wengi wanatumia kilimo cha mkono ambapo wanapata tatizo la magoti na maumivu ya Uti wa mgongo kupitia kilimo hicho.

"Taasisi hiyo ipo katika maonesho hayo kuonesha kuwa inafanya upasuaji wa kisasa za magoti na Uti wa mgongo ambapo upasuaji wa magoti hufanyika upasuaji kwa njia ya matundu," amesema Dk. Luena.

Ameongeza kuwa katika maonesho hayo ya  2022 ambayo yanabeba agenda ya 10/30 Kilimo ni Biashara Shiriki Kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi  kupitia kaulimbiu hiyo MOI inahakikisha wakulima na wafugaji wanapata elimu na ushauri ili waende kuzalisha wakiwa na afya bora.



Post a Comment

0 Comments

WAZIRI SILAA AZINDUA MNARA WA MAWASILIANO KATA YA MAKURU, SINGIDA