WAZIRI MKUU MAJALIWA AIFAGILIA CPB


 NA ASHA MWAKYONDE,MBEYA

MENEJA Masoko wa Bodi hiyo Fred Mbilinyi amesema kitendo cha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuipongeza Bodi hiyo wao kama CPB wataongeza jitihada katika maeneo aliyoyaelekeza Waziri huyo.

Pia  amewaomba  wakulima na wajasiriamali  wapeleke bidhaa zao katika Bodi hiyo Ili waziboreshe kabla hazijaingia sokoni kwa lengo  ni kuona soko la bidhaa za wakulima zikivuka mipaka nje ya nchi.

Awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza  Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB), huku  akiitaka Bodi hiyo  iendelee kutafuta masoko zaidi ndani ba nje ya nchi.

Akizungimza  akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Mbilinyi ameeleza kuwa bodi hiyo imejipanga kuhakikisha inaendelea kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ili wakulima waweze kupata soko la bidhaa zao kirahisi.

Mbilinyi Amefafanua kuwa baada ya Waziri Mkuu kupata taarifa  za Bodi inavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na kununua mazao ya wakulima,kuchakata na kuyafungasha na kutafuta masoko hatua ambayo aliridhishwa na utendaji mzuri wa kazi zao 

Meneja huyo ameongeza kuwa wajasiriamali wanapaswa kutumia fursa ya kufanya kazi na bodi hiyo ili waweze kuboresha na kuongeza thamani ya bidhaa zao kabla hazijaingia sokoni.

Mbilinyi amesema wajasiriamali wenye nia ya kufanya kazi pamoja na wao wajitokeze ili bodi hiyo iingie mkataba nao wa kuboresha bidhaa zao kabla ya kuingia sokoni ili ziweze pata kirahisi masoko ya nje.

Aidha Mbilinyi amewataka wakulima kuweza kuchangamkia fursa zinazotolewa na bodi hiyo ili waboreshe bidhaa zao kabla ya kuingia sokoni.

Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA