TARI: FAHAMU SIFA YA NDIZI AINA YA FHIA 23 KATIKA KUONGEZA KIPATO

Mtafiti Mwandamizi na Mtafiti Kiongozi wa zao la mgomba Tanzania kutoka Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI), Dk. Mpoki Shimwela akielezea ndizi aina FHIA 23 inavyoweza kumnufaisha mkulima na mfanyabishara.

NA ASHA MWAKYONDE,MBEYA

MTAFITI Mwandamizi  na Mtafiti Kiongozi wa zao la mgomba Tanzania, kutoka Taasisi ya Utafiti wa KilimoTanzania  (TARI), Dk.Mpoki Shimwela amewataka wakulima kutumia mbegu bora za migomba ambazo zimezalishwa na taasisi hiyo.
 
Akizungumza jijini Mbeya katika maonesho ya wakulima na wafugaji maarufu nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale ambapo kitaifa yanafanyika jijini hapo Mtafiti huyo amesema TARI imezalisha ndizi aina ya FHIA 23, ambazo zinaweza kumsaidia mkulima kwa usalama wa chakula na kipato. 

Mtafiti huyo amefafanua kuwa asilimia 60 hadi 70 ya ndizi zinazouzwa mjini katika mikoa ya Singida, Tabora, Dodoma ni ndizi jamii ya FHIA 23.

Ameeleza kuwa ni ndizi ambazo zinawapa kipato wakulima na wafanyabishara Wanawake na vijana huku akisema ni chanzo cha ajira na usalama wa chakula.

Mtafiti huyo kiongozi amesema kuwa  ndizi hiyo wakulima hawaivuni kwa pamoja kwa ajili ya kula bali wanavuna kwa vichane ili isiive maana akivuna kwa mara moja itamvia.

Amebainisha kuwa ndizi hiyo ina vumilia ukame inaweza kulimwa katika Kanda nyingi ambapo nyingine zinahitaji kulimwa katika mvua nyingi na unyevu nyevu huku akitolea mfano Tukuyu, Kilimanjaro na Bukoba.
 
Dk. Shimwele ameeleza kuwa ndizi hiyo kupandwa hadi kukomaa inachukua mwaka mmoja na miezi minne hadi Saba inategemea na hali ya hewa sehemu husika lakini katika sehemu za joto ndani ya mwaka mmoja na miezi mitatu hadi minne inawezwa kuvunwa.

" Ni moja ya ndizi ambazo ni zao la kujivunia TARI, ni ndizi ambazo zina uzaaji mkubwa, ukinzani wa magonjwa pamoja na wadudu, inavumilia mashambulizi ya minyoo ya migomba na bungua," amesema Mtafiti huyo.

Dk.Shimwela amesema aina hiyo ya ndizi mavuno yake ni tani 60 hadi 70 kwa kwa mwaka  na mfanyabishara anainunua kwa mkulima shilingi 20,000 lakini akiifikisha mjini anauza  zaidi ya 50,000.

Amesema kuwa upande wa uzaaji inauzao mkubwa kwa Tanzania kuliko ndizi nyingine na inaweza kutumika kwa chakula na kuivisha.

Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA