WIZARA YA KILIMO YATOA BL.80 KUDHIBITI SUMUKUVU


 NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA

SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza mradi wa kudhibiti sumukuvu wenye thamani ya shilingi bilioni 80 katika mikoa 10 na Halmashauri 18 wenye lengo la kuimarisha usalama wa chakula katika kulinda afya za jamii ndani na nje ya nchi. 

Hayo yamesemwa na Mtaalam kutoka Wizara ya Kilimo Mercy Buta katika maonyesho ya wakulima Nane Nane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja John Mwakangale Jijini Mbeya amesema mradi huo pia unatekelezwa Zanzibar katika visiwa vya Unguja na Pemba.

“Tupo katika maonesho haya hapa Mbeya kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu sumu kuvu ambayo ni sumu inayosababishwa na kuvu (fangus)," amesema Buta.

Akizungumzia madhara ya sumukuvu Mtaalam huyo amefafanua kuwa mradi huo ugonjwa wa Saratani unaripotiwa kuwa asilimia 30 inaweza kusababishwa na sumukuvu.

 "Maadhara ya sumukuvu ni halisi mtu akila chakula chenye sumukuvu kwa muda mrefu matokeo yake ni kupata kansa hivyo wakulima wanatakiwa kuwa makini katika utunzaji wa mazao yao, " amesema.Buta.

Ameongeza kuwa,katika kudhibiti sumukuvu,Wizara imekuja na teknolojia mbalimbali zinazoweza kudhibiti sumukuvu hiyo vikiwemo viuatilifu pamoja na teklojia nyingine katika kuhifadhi mazao tangu wakati wa kilimo mpaka kuhifadhi mazao.

Kwa upande wake mtaalam wa kutoka wizara ya Kilimo Hilda Shegembe ameeleza kuwa,moja ya teknolojia ni kipukuchua mahindi kwa kutumia kifaa maalumu badala ya kuweka kwenye mfuko na kupiga piga,kuyatwanga kwenye kinu ambapo kina kudhibiti sumukuvu na bei yake ni rahisi.

"Kifaa hiki ni kwa ajili ya wakulima wadogo ambao wamekuwa wakipukuchua mahindi yao kwa kuyapiga,hii ni hatari kwa usalama wa chakula kwa sababu wakati wa kuyapiga yapo yanayopasuka,yanayopasuaka husababisha wadudu wa sumukuvu kuingia katika mazao.”amefafanua.

Naye Mtaalam kutoka Wizara hiyo Pendo Nsanya amebainisha teknlojia nyingine ya kadi ya kupima unyevu ambacho kinatumika kwa kuoneakana kwa rangi zilizopo kwenye kadi hiyo.

Amesema kadi hiyo hutumika humsaidia mkulima kujua kama mazao yake yamekauka ndipo ayahifadhi badala ya kuhifadhi yakiwa mabichi na kusababisha sumukuvu kuingia katika mazao.


Post a Comment

0 Comments

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA