TEKNOLOJIA MPYA YA VETA MKOMBOZI KWA WAKULIMA


Mbunifu na Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA ),Dar es Salaam Bukuku akionyesha mashine ya kuchakata mafuta kutoka katika mbegu za mazao kama karanga, alizeti na mbegu mbegu.

NA ASHA MWAKYONDE, MBEYA

WAKULIMA na wajasiriamali wametakiwa kutembelea Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kupitia Vyuo vyake vya Ufundi Stadi ili kujifunza kwa kuwa  mamlaka hiyo inateknolojia mbalimbali za kila sekta pamoja na kuwapeleka watoto wao kusoma.

Pia VETA imebuni mashine ya kuchakata mafuta kutoka katika mbegu za mazao kama karanga alizeti na mbegu mbegu  inayojulikana kama Oil Pressor machine ambayo inatumia mikono.

Akizungimza jijini Mbeya Agosti 4, 2022, katika maonesho ya wakulima na wafugaji maarufu Nane nane yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale ambapo kitaifa yanafanyika mkoani hapa katika banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kutoka Chuo cha VETA Dar es Salaam Mwalimu na Mbunifu kutoka Chuo hicho Emmanuel Bukuku ,amesema  lengo la kubuni na kutengeneza mashine hiyo ni kupata mashine hapa Tanzania  kutokana na Watanzania kupeleka Parachichi Afrika Kusini kutengeneza bidhaa za mafuta.

Mwalimu Bukuku pia ameeleza lengo jingine ni kumsaidia mkulima aongeze  mnyororo wa thamani katika bidhaa zake.

" Maonesho ya nane nane mwaka huu tumeweza kuja na mashine ambayo inaweza kuwasaidia wakulima hasa wanaolima mazao ya kutoa mafuta kama karanga, alizeti na mazao ya mbegu mbegu mbalimbali ili waweze kutoa mafuta kwa urahisi," amesema 

Amefafanua kuwa mashine hiyo ina sehemu mbili ambapo inaweza kutengeneza mafuta ya Parachichi ambayo yanatumika kwa ajili ya kupata mwilini pamoja na nywele.

Kwa mujibu wa Mwalimu huyo sehemu ya pili mashine hiyo inaweza kutumika kutengeneza mafuta ya Kokoa.

Amebainisha kuwa mashine hiyo ina faida nyingi na ina mafanikio makubwa kwa mkulima.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU