MAFURU:IFIKAPO SEPTEMBA 23 MACHINGA WOTE WAWE KATIKA SOKO JIPYA

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Joseph Mafuru amewataka wafanyabishara ndogo ndogo maarufu Machina kuhakikia wanahamia katika soko la Machinga Complex kuanzia jana hadi ifikapo Septemba 23 wote wawewameshahamia na Septemba 24 ni siku ya kusafisha Jiji hilo.

Ujenzi wa soko hilo lililopo barabara ya Bahi umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 9.53 na  lenye uwezo kuwachukua wamachinga hao 5000 ambapo waliopo kwa sasa ni 3000.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma  Septemba 7,2022, Mafuru wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema kukamilika kwa soko la machinga ni kielelezo tosha cha kulifanya jiji hilo kuwa katika mpangilio mzuri ambao unaendana na makao makuu.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa Halmashauri hiyo imetumia mapato yake ya ndani kiasi cha shilingi bilioni 6.5 katika ujenzi huo wa soko ambapo Rais Samia Suluhu Hassan aliwapatia bilioni 3.

katika soko hilo huduma zote muhimu zipo zikiwamo kituo cha Polisi kuhakikisha ulinza na usalama wa wafanyabishara hao na wateja wao unakuwepo, sehemu ya kuwanyonyeshea Watoto, baa pamoja na kamera za CCTV.

Aidha Mafuru amesema jiji hilo hutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo Kila Mwaka kiasi Cha Shilingi bilioni 1 na tayari wametenga bilioni 5 kwaajili yakuwakopesha wafanyabiashara hao.

Ikumbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan alitoa kiasi cha Billion 3 ikiwa ni juhudi za kuendeleza ujenzi wa soko hilo na hatimae limekalika.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU