UJENZI WA MAABARA YA TAIFA YA TAEC WAFIKIA ASILIMIA 85

 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stanlaus Nyongo,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),yanayojengwa Kikombo jijini Dodoma Septemba 8,2022.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kutembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa taasisi hiyo inayojengwa Kikombo jijini Dodoma Septemba 8,2022.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),Prof.Lazaro Busagala,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kutembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa taasisi hiyo inayojengwa Kikombo jijini Dodoma Septemba 8,2022.

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Huduma za maendeleo ya Jamii,imeridhishwa na ujenzi wa Maabara ya Taifa ya TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), huku ikiiagiza tume hiyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ifikapo Septemba,30 Mwaka huu ili ianze kutumika kwa manufaa ya Umma na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua Maabara na Ofisi za Tume hiyo katika Kata ya Kikombo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma,Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stanlaus Nyongo amesema kuwa ujenzi wa maabara hiyo umefikia asilimia 85.

Nyongo amesema kuwa thamani ya Fedha ya shilingi bilioni 3.8 iliyotumika katika ujenzi wa maabara hiyo imeonekana huku akisema kujengwa kwa ofisi na kuhamia Jijini Dodoma kutarahisisha wananchi kupata huduma kwa urahisi na ukaribu kwani huduma hiyo ni muhimu kwa Usalama wao na usalama wa Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa uwepo wa Maabara hiyo itarahisisha upimaji wa baadhi ya bidhaa ambazo zinazotumia mionzi ikiwemo na suala la usalama wa nguvu za Atomiki kwa ujumla.

Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Maswa Mashariki ameitaka Tume hiyo ya nguvu za Atomiki kwakushirikiana na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia iwaambie watanzania kwa kutoa Elimu kuhusu huduma wanazotoa kwa lengo la kufahamu na kuitumia Maabara hiyo.

Naye Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema amepokea maelekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma Za maendeleo ya Jamii na kuahidi kuyatekeleza kwa wakati na kwamba Tume ya nguvu za Atomiki ni muhimu hasa katika suala la usalama wa nchi na kuahidi kuendelea kuwekeza katika Ofisi zote za Kanda za Tume hiyo..

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Atomiki Profesa Lazaro Busagara ameeleza faida ya Maabara hiyo pindi itakapokamilika ni pamoja na kuendeleza uzalishaji wa Sekta ya nyuklia Nchini.

Prof.Lazaro Busagala, amesema kuwa ujenzi huo unahusisha maabara na ofisi za taasisi hiyo pindi itakapohamisha makao yake Dodoma.

Amesema kumiliki ofisi itasaidia kuounguza gharama za kupangisha ofisi hivyo kuokoa fedha nyingi za serikali ambazo zingetumika katika upangishaji wa ofisi.

Tume ya nguvu ya Atomiki ambayo ipo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa Sasa Makao Makuu yake yapo Mkoani Arusha.

Kazi yake kubwa ni kudhibiti matumizi mabaya ya mionzi.






Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI