UZINDUZI WA MKAKATI WA KUIMARISHA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI NGAZI YA ELIMU HALMASHAURI YA CHAMWINO


 NA MWANDISHI WETU

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Chamwino Bi.Neema Nyarege amewataka wakuu wa shule za msingi kuwaandaa kikamilifu watahiniwa ili waweze kupata ufaulu wenye tija wa daraja A mpaka C na kuondoa ufaulu wa alama D na E kwa ngazi ya shule za msingi.
 
Bi.Nyarege ametoa tamko hilo wakati akizungumza na maafisa elimu msingi na sekondari,wakuu wa idara,maafisa elimu kata na wakuu wa shule kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe.Gift Msuya kwenye uzinduzi wa kukabidhi mkakati wa kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji katika ngazi ya elimu msingi tarehe 09.09.2022 wilayani Chamwino.
 
Amesema kuwa katika shule za sekondari nazo zinatakiwa kuongeza ufaulu wa daraja la 1hadi 3  na kupunguza au kuondoa kabisa ufaulu wa daraja la 4 na daraja sifuri.
 
"Viongozi wa Elimu wasimamie nidhamu kwa wanafunzi na watumishi katika kuimarisha zoezi la ujifunzaji na ufundishaji katika taaisis zote aidha ushauri nasaha utolewe kwa wanafunzi ili waweze kukabiliana na changamoto watakazo kutana nazo katika ujifunzaji "amesema hayo Bi.Nyarege
 
Aidha Bi.Nyarege amesema kuwa wanafunzi watoro watambuliwe na warudishwe shuleni kupitia watendaji wa vijiji na Taarifa zitumwe katika ofisi ya mkurugenzi kila ijumaa kabla au ifikapo saa 4 asubuhi ili ziweze kutumwa mkoani na wiki ya pili au inayofuata taarifa za idadi ya wanafunzi watoro waliorudi shuleni ziwasilishwe.
 
"Ninafahamu kuwa Mwongozo ulizinduliwa rasmi tarehe 04.08.2022 mkoani Tabora na waziri mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa alizungumzia malengo ya mwongozo wa uandikishaji wanafunzi darasa la kwanza ili kuhakikisha wanafunzi walioandikishwa wanamaliza elimu ya msingi kama waivyoanza"Amesema hayo Bi.Nyarege
 
Pia amesema kuwa viongozi katika ngazi zote wahakikishe walimu wanatambuliwa,kuthaminiwa na kuwezeshwa pamoja na kushirikishwa,kutiwa moyo na kutobaguliwa huku akiwataka wazazi kuwaheshimu walimu ,kuwatambua na kuwapa ushirikiano.
 
Mbali na hayo amewataka walimj kuonyesha ushirikiano na kujitathimini huku akitaka uteuzi wa viongozi wa elimu kutingatia weledi ,uzoefu na ubunifu katika ngazi zote.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI