GCLA YABORESHA MFUMO WA UTOAJI HUDUMA KWA NJIA YA MTANDAO MAABARA BILA SHAHIDI KWENDA MAHAKAMANI


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),imefanya maboresho kwa kujenga mfumo wa kuwaunganisha  Wadau wote ili waweza kupata taarifa za matokeo ya nini kinachoendelea katika Maabara hiyo.

Pia Maabara hiyo ina ithibati  ya kimataifa ambayo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Tanzania ni nchi  ya kwanza na kwa ukanda wa Sahara ni ya nne baada ya Afrika Kusini, Mauritius ma Botswana.

Akizungumza Jijini Dodoma leo Januari 25,2023, katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square, Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai wa GCLA, David Elias amesema maboresho mengine ni utoaji wa ushahidi kwa mfumo wa mtandao.

Mkurugenzi huyo amesema  kwa sasa utoaji wa ushahidi unatumika ni Kwa njia ya  mtandao wa Maabara unaolenga  kutoa ushahidi pale pale ofisini pasipo shahidi kwenda mahakamani.

 
"Kamishna  wa DCEA, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu inatoa matokeo ambayo  inakubalika kitaifa na kimataifa pia tuna mashahidi 11 ambao wametambuliwa kitaifa na kimataifa unaweza kuwatumia katika ushahidi," amesema Elias.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa wamepeleka huduma katika  Kanda sita  na kwamba Kanda ya kati ni Dodoma,Singida,Iringa pia Kanda ya ziwa  Mwanza na Kanda ya Kaskazini Arusha Kanda ya Kusini Mtwara na Kanda ya Juu Kusini Mbeya.

Ameongeza kuwa Kanda zote hizo wanawatoaji wa ushahidi kwa njia ya mtandao na kwamba wamesongeza huduma hizo lengo likiwa ni kutoa haki kwa wote na kwa gharama nafuu zinazopatikana kwa kusogezewa huduma hizo.


Kwa upande wake, Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Gerald Kusaya ameipongeza GCLA kwa kazi nzuri wanazozifanya na kusema kuwa na  wao wanafarijika kwa jinsi ambayo wanazidi kushirikiana.

"Ushirikiano huu naomba uendelee kudumu lakini lengo letu kama mnavyofahamu sisi mamlaka ni kuwatumikia Watanzania yale yanayowezekana ndani ya uwezo wetu tufanye katika ufanisi bila kumuonea mtu," amesema.

Ameongeza kuwa wao wapo kwa ajili ya kutenda haki na kwamba wanaiamini mamlaka ya Mkemia Mkuu wa serikali.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU