Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepeleka timu ya watu watatu mkoani Kilimanjaro ili kufuatilia taarifa ambazo zimetoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu Shule zinazofundisha watoto tabia mbaya za kulawitiana.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya baadhi ya vyombo vya habari kutoa faarifa zinazohusu wanafunzi kufundishwa kulawitiana.
Akizungumza jijini Dodoma leo Janauari 17,2023 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameeleza kuwa wizara imeshutushwa na taarifa hizo imepeleka timu na kwamba wanapenda timu hiyo ihakikishe wana ukweli wote ili wizara iweze kuchukua hatua stahiki.
Prof.Mkenda ameitaja timu hiyo iliyopelekwa kuwa ni kamishna wa elimu,Mkurugenzi wa udhibiti ubora pamoja na mwanasheria wa wizara huyo.
"Kuna taarifa ambazo zimetoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu Shule zinazofundisha watoto tabia mbaya za kulawitiana,tumezichukua kwa umuhimu mkubwa sana," Ameongeza.
Taenda kamishna wa elimu mwenye sio mwakilishi wake,Mkurugenzi wa udhibiti ubora mwenyewe sio mwakilishi wake pamoja na mwanasheria wa wizara aende haraka sasa hivi wanapitia hizo Shule zilizotajwa na kujaribu kupata ukweli wote," amesema Prof. Mkenda.
Kwa mujibu wa Waziri hiyo tumeongea na Mkuu wa Mkoa husika kumuomba asaidiane na timu hiyo kwenda kule pamoja na kusaidia ili kama kuna sehemu yenye makosa ja jinai polisi wachujue hatua mara moja.
Ameongeza kuwa wanatarajia walioenda wataleta taarifa kamali na kwamba wizara ipo tayari kuchukua hatua stahiki kudhibiti mambo hayo.
Prof. Mkenda amesema kwa kuwa suala hilo limetokea katika eneo moja kunaweza kukawa na taarifa maeneo mengine hivyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo kesho atatangaza namba ambayo mtu yoyote akijua kuna kitu kama hicho katika shule yoyote hapa nchini Shule za Umma, binafisi au Vyuo vyovyote anawezakupiga simu na kutoa taarifa na wizara hiyo kuweza kufuatilia kwa nchi nzima.
Amesema kuwa wanaongeza umakini wa kufuatilia mambo hayo kwa kuwa yanaweza kuchafua Wizara ya elimu, yanaharibu vijana na kusababishia wazazi wakose imani na shule.
Prof. Mkenda amefafanua kuwa hivi karibuni waliketi kikao cha kujadili na kuanza mkakati wa kitaifa wa kuangalia namba ya kudhibiti vitendo hivyo vya kulawitiana ambayo vinatokea shuleni, nyumbani, njiani na sehemu mbalimbali hapa nchini.
Prof. Mkenda ameeleza kuwa suala hilo sio la wizara moja ni suala mtambuka na kwamba kazi inaendelea na makatibu Wakuu watarudisha taarifa yao na watakuwa na mkakati mzuri zaidi wa utekelezaji wa kitaifa.
0 Comments