DMI KUWATAFUTIA AJIRA WANAFUNZI WAO


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

CHUO cha Bahari Dar es salaam (DMI),
kimefanikiwa kuwaunganisha na waajiri mabaharia 27, kupata ajira na mafunzo kwa vitendo kutokana kuanzisha utaratibu wa kujenga uhusiano na wamiliki wa meli  lengo likiwa ni kupata  nafasi hizo za ajira na mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya mabaharia hao wa kitanzania nje na ndani ya nchi.

Pia DMI kinampango wa kuboresha karakana ya mafunzo kwa kuongeza vifaa na maeneo ya kujifunzia kuwa ya kisasa zaidi ili kuendana na mabadaliko ya sayansi na teknolojia pamoja na soko la ajira.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Februari 9,2023 na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho ,Dkt.Tumaini Gurumo  wakati akizungumza na waandishi wa habari kueleza utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho, ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita imewezesha kupata maeneo mbalimbali ya kujenga matawi ya DMI katika Mikoa ya Lindi na Mwanza.

Ameongeza kuwa matawi haya yatakapo kamilika huduma ya elimu na mafunzo ya usalama wa vyombo vya usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji itakuwa imesogezwa karibu zaidi na wananchi.

"Matawi haya yatawezesha vijana wengi zaidi kupata elimu na kupanua wigo wa ajira kwasababu soko la ajira ya ubaharia nchini linaendelea kuongezeka na katika ulimwengu ni kubwa kwa sasa," amesema.


Akizungumzia  mipango mingine ya Chuo hicho amesema ni pamoja na kujenga vyombo vidogo vidogo vya usafiri majini ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo,kujenga miundombinu ya chuo kwa viwango vya juu mkabala na ufukwe wa bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam ilikukidhi mahitaji ya ongezeko la wanafunzi,walimu na kozi.

Amesema pamoja na kupeleka elimu na mafunzo ya ubaharia katika maendeleo mengi zaidi ya nchi yetu ikiwemo Pemba na Kigoma.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI