WHI KUPITIA KITENGO CHA UJENZI IMELIPA GAWIO LA BILIONI 1.01 KWA WAWEKEZAJI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 4

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WATUMISHI Housing Investment( WHI),imeweza kuanzisha kitengo cha Ujenzi na ushauri na katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 na kupata leseni ya mkandarasi daraja la 1 kupitia kitengo hicho imejenga Majengo ya serikali.

Pia Bodi ya Watumishi Housing Investment
pamoja na ubunifu wa wafanyakazi wamefanikiwa kushusha bei za nyumba kwa kati ya asilimia 10 hadi 30 na kuwafanya watumishi wa umma na wanachama wa mifumo ya hifadhi ya jamii kuweza kununua nyumba zilizojengwa kwa kutumia mishahara yao.

Akizungumza Jijini Dodoma Februari 9,2023, katika kuelekea utekelezaji wa majukumu ya WHI, Mkurugenzi Mkuu wa  Taasisi hiyo Dk.Fred Msemwa amesema kuwa kupitia kitengo hicho Ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zaidi umewekezwa,kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita.

Mkurugenzi  huyo amesema kuwa WHI imeweza kulipa jumla ya gawio la shilingi Bilioni  1.01 kwa wawekezaji wake na kuchangia Mfuko mkuu wa Serikali jumla ya shilingi Milioni 50.

Ameeleza kuwa kabla ya kuanzishwa kwa Watumishi Housing Investment kulikuwa na changamoto ya kupata makazi haswa kwa watumishi wa umma,wafanyakazi na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii walikuwa wanashindwa kununua nyumba kwa kutumia mishahara yao.

Dk.Msemwa ameongeza WHI
imefanikiwa kuwauzia nyumba walimu,wauguzi,madaktari,maofisa wa kawaida katika utumishi wa umma ambao tayari wamenunua na wanaishi katika nyumba zilizojengwa na watumishi housing maeneo mbalimbali Nchini.

Mkurugenzi huyuo ametolea mfano katika mradi wa magomeni uliopo katika Jiji la Dar es salaama ambalo  wameuza nyumba 88 kwa watumishi wa umma wakiwemo madaktari wa Hospitali ya muhimbili na wauguzi ambao sasa wanaweza kufika katika vituo vyao vya kazi kirahisi na kuwahudumia watanzania,

Amesema WHI imejenga nyumba 175 na kuziuza kwa watumishi wa umma waliohamia Jijini Dodoma na kati ya hizo nyumba 30 zimeunzwa kwa Chuo kikuu cha Dodoma na zinatumiwa na wahadhili wa Chuo hicho. 

Dk.Msemwa ameongeza kuwa Watumishi Housing ilishirikiana na mamlaka ya elimu yaani TEA kujenga nyumba 186 vijijini katika shule za Kata zenye mazingira magumu,mradi huo wa nyumba za walimu umekuwa na manufaa makubwa katika kuwawezesha walimu kupata makazi bora.

"Miongoni mwa mafanikio toka kuanzishwa kwa WHI ni pamoja na kujenga nyumba 983 katika maeneo mbalimbali na kuuzwa kwa watumishi wa umma na wanachama wa Mifuko ya hifadhi ya jamii,tangu kuanzishwa kwakwe imepata hati safi ya hesabu kila mwaka kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu(CAG),imetekeleza Ujenzi wa nyumba na Ofisi za taasisi mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri elekezi," amesema.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI