Na Asha Mwakyonde,Dodoma
MAMLAKA ya kusimamia uvuvi wa Bahari Kuu imesema kuwa katika kutekeleza mikakati yake inatarajia Kujenga Kiwanda kikubwa Cha kuchakata Samaki Mkoani Tanga ambacho kitakuwa na uwezo wakuzalisha Tani zaidi ya 100 hadi 200 kwa siku .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,Dk Emanuel Sweke ameyasema hayo February 8,2023 jijini hapa wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya usimamizi wa Bahari Kuu mbele ya Waandishi wa Habari amesema kiwanda hicho kitagharimu Dola Milioni10 .
Amesema kuwa kiwanda hicho pindi kitakapokamilika kitaweza kutoa fursa ya ajira kwa vijana 100 wa kitanzania.
Mkurugenzi huyo akizungumzia suala la kudhibiti uvuvi haramu amesema Mamlaka hiyo imeweza kuweka mifumo madhubuti ambayo inaendana na Teknolojia kwakufanya doria mbalimbali kwajili ya kukomesha suala la uvuvi haramu.
" Mifumo inasaidia kujua nani anafanya kosa na ikitokea mtu amezima mifumo atajulikana tu kama yupo eneo gani la bahari ya Tanzania," ameeleza Mkurugenzi Dk Swake.
Amesema katika hatua nyingine amesema kuwa kutokana na shughuli zake Mamlaka hiyo imeweza kuvunja rekodi ya kukusanya Mapato mengi kwa Kipindi Cha 2022 hadi kufikia Shilingi Bilioni4.1 huku akisema hadi Sasa wametoa jumla ya leseni za uvuvi 536.
Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa Bahari Kuu imeanzishwa rasmi Mwaka 2010 lengo lake likiwa ni kusimamia shughuli zote za uvuvi wa Bahari Kuu na ufuatiliaji.
0 Comments