Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye
amesema kuwa ameshangazwa na kauli ya viongozi Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF),kutoka na kuongea kwa jaziba mbele ya vyombo vya habari wakati walikuwa pamoja tangu mwanzo
Hata hivyo amelaani vikali kauli hiyo iliyotolewa na TEF Februari 8,2022, kuhusu mchakato wa marekebisho ya sheria za huduma ya habari kwamba inapigwa danadana ambapo ameeleza kauli waliotoa ni kauli ya chuki na za kuvunja moyo.
Akzungumza na waandishi wa habari Februari 9,2023, jijini hapa Waziri huyo ameesema jukwaa hilo limezungumza hadharani maneno ya kuvunja moyo.
Waziri Nape amefafanua kuwa kwa mujibu wa maelezo ya TEF Muswada huo umekuwa na danadana na kwamba hata ukisoma na kusikiliza zaidi inaonyesha Serikali imevunjika vipande vipande.
Amesema kuwa wamefanya kazi kwa pamoja na jukwaa hilo tangu mwanzo mwa mchakato huo hadi hapa walipofikia hivyo huku akitamani ushirikiano huo uendelee.
Aidha amewataka kukumbuka kuwa sheria sio ya mtu fulani ni yawatu wote hivyo tuwe na imani zoezi hili litaisha pamoja.
KAULI YA TEF
Februari 8, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) likisikika likisema limepokea kwa mshituko makubwa kauli ya Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kuwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari (MSA 2016) umeshindikana kuingizwa bungeni kutokana na ripoti nyingi za Kamati za Kisekta za Bunge.
TEF imeona sababu iliyotolewa ni nyepesi na inapata wasiwasi iwapo kuna utashi wa kufanya mabadiliko katika sheria hii.
Aidha wamesema Katika vikao vilivyotangulia, waliona ugumu kutoka kwa baadhi ya maofisa wastaafu walioazimwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), maafisa kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,na baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama wakionesha wazi kutokuwa na nia ya kurekebisha sheria hii.
Wamesema Mara kadhaa vikao vilivyofanyika, viliisha bila mwafaka katika vifungu mbalimbali ikiwamo Mamlaka ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) chini ya vifungu vya 9 na 10, ambavyo vinampa mamlaka ya kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka, mtoa hukumu na msimamizi wa utekelezaji wa hukumu;suala tunalosema ni ukiukwaji wa Utawala Bora na Utawala wa Sheria.
0 Comments