MSIGWA AWAPA TOMA JUKUMU LA KUHAKISHA HABARI ZA MTANDAONI ZINAKUWA NA WELEDI


 Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amewataka waandishi wa habari mtandaoni kuzingatia uweledi  wa taaluma yao ikiwa ni pamoja na kutotumika na watu, makundi venye uovu vyenye nia mbaya kwa Taifa.

Pia Serekali imewataka wadau wa masuala ya habari na wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia weledi katika utendaji kazi wao hasa katika kipindi hiki cha Mapinduzi ya teknolojia na maudhui yanazingatiwa kuendana na taaluma hiyo.

Akizungumzia jijini Dodoma,Februari 10,2023,wakati akizindua Taasisi ya Waandishi wa Habari za Mtandaoni (TOMA),Msingwa ameeleza kuwa ili kujitofautisha  na wanaotaka kuwatumia wanaandishi  kwa maslahi  yao binafisi ni vema kulinda taaluma ya Habari.

Msingwa amesema Serikali inaona na kutambua  juhudi za vyombo vya habari hali iliyosababisha kutoa uhuru wa kutosha kwa kila mmoja kuanzisha na kumiliki chombo cha habari ila lakini changamoto katika uchujaji ni kipi kiende hewani na kipi kisiende kulingana na maudhui yake.

Ameongeza kuwa kutokana na Teknolojia kukua Tasnia ya Habari imekuwa nguzo kubwa kwa sekta ya habari nchini huku akitoa angalizo kwa  kadiri zinavyoongezeka inaonekana kama weledi wake unapungua .

Aidha amewataka TOMA kuhakikisha waandishi wa habari mtandaoni wanakuwa na uelewa mkubwa juu ya machapisho wanaotuma mtandaoni kwa kuwa imekuwa tegemeo kama chanzo kikuu cha habari.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI