BUWSSA YAPITISHIWA MIRADI YENYE BIL.28.1 KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA DK. SAMIA


Na Asha Mwakyonde DODOMA 

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda(BUWSSA), imepitishiwa miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 28.1 tangu awamu ya sita kuanza na kwamba shilingi bilioni 11tayari zimepokelewa na kwamba baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea.

Pia mamlaka hiyo ina ujenzi wa mradi wa miundo ya majitaka katika eneo la Butakale kwa ajili ya usafi wa mazingira, mradi huo unatarajia kukamilika kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025.

Akizungumza jana jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo Esther Gilyoma wakati akielezea mafanikio,mikakati na Mipango ya BUWSSA ndani ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan alisema mradi huu una ununuzi wa magari mawili ya majitaka yenye uwezo wa kubeba lita 10,000 na 5,000.

Mkurugenzi Mtendaji huyo ameeleza kuwa Mamlaka ina mipango mbali mbali kwa ajili ya kuhakisha huduma inazidi kuinaimarika mjini Bunda kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Amezitaja Mipango hiyo kuwa ni uenzi wa mfumo wa wa mtandao wa maji taka,ujenzi wa tangi kubwa la maji lenye uwezo wa kubeba lita 670,000 kwenye kituo cha kusukuma maji pamoja na ujenzi wa tangi kubwa lenye uwezo wa kubeba lita 225,000 kwenye kituo cha kusukuma maji Mugaja.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mipango mingine ni ujenzi wa tangi la maji lenye uwezo wa kubeba lita 150 Kisangwa,ujenzi wa upanuzi mtandao wa bomba 300mm toka Migungani hadi Mlima bomani na ujenzi wa mtando wa bomba toka kituo cha kusukuma maji Migungani hadi mlima Nyiendo.

Amesema mikakati ya mamlaka hiyo ni kuwa na mfumo wa majitaka wa bomba ili kuzidi kuweka mazingira ya Mji wa Bunda salama, kuongeza uwezo wak uhifadhali maji hasa pale umeme unapokatika na kusababisha huduma kusimama na kupunguza vituovya kusukuma maji ili kupunguza gharama za umeme.

Ameongeza kuwa Mlmikakati mingine ni kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji kituo cha kusukuma maji Migungani, kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji kituo cha kusukuma maji Mugaja Wananchi wa Kisangwa waweze pata maji kwa njia ya mseleleko.

Pia mkurugenzi Mtendaji huyo alieleza kuwa kuongeza uwezo wa kusukuma maji mengi mjini Bunda kwa kutumia pampu mbili Kuongeza wingi wa majim jini Bunda.

"Upotevu wa maji kwa mwaka 2021 ulikuwa watani wa asilimia 64 kutokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kuanzia mwaka 1972, baada ya jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya sita za kutoa fedha za kubadili bomba chakavu na mita goigoi upotevu wa maji kwa sasa ni asilimia 32 na unaendelea kushuka kutokana na jitihada zinazoendelea kufanyika," amesema.

Amefafanua kuwa kwa sasa Mamlaka hiyo inatoa huduma ya majisafi kwa wastani wa masaa 22 bila ya kuwa na mgawo wa maji, baada ya miradi miwili kukamilika ambayo kwa sasa inaendelea mradi wa kusambaza maji Wariku na mradi wa maji Kisangwa.

Gilyoma amesema itatoa huduma ya maji kwa masaa 24 na kufikisha wastani wa utoaji wa huduma kwa wastani wa asilimia 96 na kufikia lengo la ILANI yaChama Cha Mapinduzi (CCM).

Post a Comment

0 Comments

UDOSO SCHOLARSHIP FUND YAZINDULIWA