Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akifafanua jambo katika kikao na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright hayupo (pichani).
Na Mwandishi wetu Dodoma
SERIKALI ya Marekani inatarajia kuipatia Tanzania Dola za kimarekani milioni 5 kwa ili kufanikisha mpango mpya wa Vaccine wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa chanjo nchini ambapo itamsaidia kuwalinda Watanzania na maambukizi dhidi ya UVIKO-19.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo Februari 2, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright.
Katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.
Katika kikao hicho wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kwa upande wa sekta ya afya pamoja na kuainisha vipaumbele vyao kwenye eneo la afya kinga hususani eneo la mama na mtoto, lishe, masuala ya chanjo.
Pia kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kusisitiza uhamasishaji wa elimu ya afya kwa umma.
Waziri Ummy amebainisha kuwa kwa kutumia mfumo wa jamii shirikishi katika utoaji wa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 maeneo ya huduma za umma utasaidia kuwafikia watanzania wengi kupata chanjo.
Kwa upande wake Balozi Wright amesema ushirikiano uliopo baina ya nchi yake na Serikali ya Tanzania ameahidi kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 5 kwa Serikali ya Tanzania lengo likiwa ni kufanikisha mpango mpya wa Global Vaccines wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa chanjo nchini ili kuwalinda watanzania na maambukizi dhidi ya Uviko-19.
Mbali na hayo Balozi Wright ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa namna inavyokabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19 kupitia kuelimisha wananchi kuchukua hatua stahiki zinazoshauriwa na wataalam.
Aidha Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Marekani kwa ushirikiano wa muda mrefu na ameahidi kuimarisha zaidi ushirikiano kwa faida ya nchi zote mbili.
0 Comments