Baadhi ya wajasiriamali kutoka vikundi 78 wakikabidhiwa hundi kuashiria kupatiwa fedha za kuendeleza miradi ya vikundi vyaoNa Asha Mwakyonde, Dodoma
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma la
imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 817,400,000 kwa vikundi 78 vya ujasiriamali ikiwa ni fedha za ndani za Halmashauri hiyo katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka.
Pia wajasiriamali hao wametakiwa kuitumia mikopo hiyo kuitumia katika kuwaletea mabadiliko ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na kwa jamii kwa ujumla.
Akizungumza leo Febuari 3, 2022 jijini hapa wakati akikabidhi mikopo kwa wajasiriamali hao Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amesema mikopo hiyo ni pamoja na lori aina ya fuso tani saba kwa ajili ya kubebea mchanga na matofali, Guta.
Mkuu huyo wa Wilaya amefafanua kuwa fedha hizo ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ambayo yanatakiwa kurejeshwa kama mkopo kwa Vijana, Wanawake, na Watu Wenye Ulemavu.
"Pia tumetoa mikopo kwa ajili ya biashasha ndogondogo,mikopo ya kilimo,mifugo na mikopo kwa ajili ya mama lishe na baba lishe, amesema Shekimweri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji hilo Joseph Mafuru amesema kuwa wametoa fedha hizo ikiwa ni utekelezaji sera ya kutoa asilimia kumi kwa makundi ya vijana,akina mama na watu wenye ulemavu.
"Mikopo hii tunatoa kwa vijana asilimia nne, akina mama asilimia nne na kwa watu wenye ulemavu asilimia 2 lengo lake ni kuwawezesha ili waweze kujikwamua kiuchumi na wasiwe tegemezi," amesema Mafuru.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa
halmashauri ya Jiji hilo kwa kipindi cha mwaka wa fedha imetoa jumla ya mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.87.
Amefafanua zaidi kuwa taarifa inaonesha shilingi 3,981,070,933.62 tu ndizo zimerejeshwa ambapo ni sawa na asilimia 44.9 ya kiasi cha mikopo iliyotolewa.
Mafuru amefafanua kuwa mikopo iliyotolewa leo vikundi 46 vya wanawake wamepata milioni 395, 000,000 vikundi 23 vya vijana nao wamepatiwa milioni 364,000,000 na vikundi 19 vya watu wenye ulemavu wamepata sh.58,400,000 na kufanya jumla ya vikundi 78 kupata jumla ya fedha sh.817,400,000.
Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Ilumbo Group Monica Masado amesema kikundi hicho kimekuwa wanufaika wakuu wa mikopo inayotolewa halmashuri hiyo.
Naibu Meya wa Jiji la Dodoma Emmanuel Chibago amewasisitiza wakopaji hao kufanya shughuli za maendeleo badala ya kukopa na kutumia fedha hizo kwa matumizi mengine.
0 Comments