DK. GWAJIMA ATAJA MAFANIKIO YA WIZARA YAKE KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA





Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Wizara katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima kaizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Wizara katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mwanaid Ali Khamis kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amon Mpanju.


Baadhi ya wakurugenzi kutoka WIzara ya na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Wizara katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan imewajengea watoto 250 Makao Makao ya Taifa ya watoto yaliopo Kikombo jijini Dodoma yenye thamani ya shilingi bilioni 12.7 wanaohudumiwa na makazi hayo.

Pia Serikali hiyo imewatambua rasmi wafanyanyabiashara ndogo ndogo (Wamachinga),kuwa kundi maalumu na Februari,22 hadi 23 mwaka huu wizara hiyo iliandaa semina elekezi iliyojumuisha viongozi 10 kutoka Shirikishi la Umoja wa Wamachinga (SHIUMA), ngazi ya Taifa pamoja na viongozi 78,wa mikoa 26 ambayo ilifanyika jijini Dodoma.

Hayo yamesema  jijini Dodoma leo Machi 28 na waziri wa wizara hiyo Dk. Dorothy Gwajima wakati akizungumza na waandishi wa Habari
alipokuwa akizungumzia mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais huyo  amesema tayari ameshaunda Kamati ya kitaifa ya ushauri  yenye Wajumbe 25 kutoka Pande mbili za Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar) na kufanya uzinduzi jijini Dodoma  Desemba16, 2021.

Amesema hiyo ni katika kutekeleza ajenda ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia na malengo ya jukwaa la kimataifa la kizazi chenye Usawa na kwamba Rais Samia  tayari ameshaunda Kamati ya kitaifa ya ushauri  yenye Wajumbe 25 kutoka Pande mbili za Muungano (Tanzania Bara na Zanzibar) na kufanya uzinduzi jijini Dodoma  Desemba16, 2021 katika kipindi cha mwaka wake mmoja.

Ameongeza kuwa wamepata mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kukabiliana na vitendo vya ukatili ambapo hadi kufikia Februari 2022, ambapo  jumla ya Madawati saba yameanzishwa katika Taasisi za  Saba za  elimu .

Waziri huyo amezitaja taasisi hizo kuwa  ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Taasisi ya Ustawi wa Jamii na Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya cha Bugando.

" Katika kipindi cha Machi 2021 hadi Februari mwaka huu  Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto 1,843 zimeanzishwa na kufanya idadi ya kamati za hizi kufikia 18,186 kati ya Kamati 20,750 zilizokusudiwa kuanzishwa kuanzia ngazi ya Kijiji/Mtaa hadi Taifa ifikapo Juni 2022," amesema.

 Dk. Gwajima amefafanua katika kukabiliana na upungufu wa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii Tasisi ya Manedeleo ya Jamii Kijitonyama, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Vyuo vya Maendeleo ya  Jamii na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Ufundi vimeendelea kutoa elimu kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada ambapo Mwaka 2021/22, jumla ya wanafunzi 5,014 wa fani ya maendeleo ya jamii na wanafunzi 3,234 wa fani ya ustawi wa jamii walidahiliwa kwa mujibu wa vigezo vya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Ameeleza kwamba jumla ya wanafunzi 4,500 walihitimu katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Vyuo sita (6) vya Maendeleo ya Jamii vya Buhare, Rungemba, Ruaha, Uyole, Mlale na Monduli pamoja na Vyuo viwili (2) vya Maendeleo ya Jamii Ufundi vya Misungwi na Mabughai. Aidha, jumla ya wanafunzi 2,493 walihitimu katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Kijitonyama.

Pia amesema  wamefakiwa kwa kuhamashisha jamii katika ujenzi wa nyumba bora ambapo zimeongezeka kutoka nyumba 751 mwaka 2020 hadi kufikia nyumba 3,257 Februari 2022 ambapo nyumba hizo zilizojengwa Mikoa ya Arusha, Morogoro, Songwe, Shinyanga, Pwani, Katavi, Mtwara, Singida na Mwanza.

Aidha ameeleza kuwa  mafanikio hayo, Wizara imeendelea kusimamia uanzishaji na uendeshaji wa huduma za vituo vya kulelea watoto wachanga na watoto wadogo mchana, ambapo katika kipindi cha Machi 2021 hadi Februari 2022, Wizara imefanikiwa kusajili vituo 303 vilivyodahili watoto 6,772 ambapo wanaume ni  3,194 na wanawake ni 3,578.

Waziri Gwajima amesema vituo hivyo vimewezesha watoto kupatiwa huduma zinazochochea uchangamshi wa awali wa makuzi kimwili, kiakili, kihisia, kijamii na ukuaji wa lugha pamoja ikiwa ni maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu CCM Kifungu 93 (A na D na F).

"Tayari Serikali imekamilisha uundaji wa Mabaraza ya Wazee katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na kisha kuunda Baraza la Taifa la Wazee na hivyo kufikia lengo la kuwa na Mabaraza 20,749 na uwepo wa mabaraza haya imesaidia kupunguza mauaji ya wazee kutoka 190 mwaka 2015 hadi 54 kufikia Februari, mwaka huu, " amesema.

Amesema serikali imewezesha kuongezeka kwa bajeti ya Wizara kutoka Shilingi 33,195,738,400 Bilioni, mwaka 2020/21 hadi Shilingi 43,625,929,000 Bilioni, mwaka 2021/22 ikiwa ni ongezeko la Shilingi 10,430,190,600 sawa na asilimia 31.



Post a Comment

0 Comments

THBUB YAHIMIZA WANANCHI NA WATUMISHI KUHESHIMU MISINGI YA UTAWALA BORA