SERIKALI YA MAREKANI NA TANZANIA ZA SHIRIKIANA KUZINDUA BWENI LA WASICHANA ROYOLA

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sanyansi na Teknolojia Prof. Jamey Mdoe, akizindua Jengo la Bweni la wasichana shule ya sekondari Loyola.

NA MOSES MWAKIBOLWA,DAR ES SALAAM

SERIKAI ya Marekani kupitia Shirika la USAID -ASHA kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania,  imefanya uzinduzi wa Bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Loyola lenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi wapatao 456.  Ufunguzi huo ulishughudiwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali, viongozi wa dini, makampuni binafsi  wakiwemo, mheshimiwa Profesa James Mdoe aliyemwakilisha Waziri wa Elimu, mkuu wa wa Wilaya ya Ubungo Hery James na Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo (MB) na Hery Mchamungu Askofu msaidizi Jimbo la Dar la Dar Es Salaam 

Wakizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Bi. Kate Somvongsiri na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe walihudhuria hafla ya kukata utepe wa bweni hilo jipya la wasichana. Ujenzi wa mabweni mapya ya Shule la Sekondari Loyola lenye thamani ya dola za kimarekani 772,000 sawa na 
 shiling bilioni 1.8 za kitanzania ulifadhiliwa na Shirika la USAID kupitia mpango wake wa Shule na Hospital za nchi za nje na utahudumia wasichana 400.

Mkurugenzi huyo wa USAID amesema ukosefu wa usawa wa kijinsia bado unaoendelea  nchini Tanzania na  licha ya juhudi kubwa zinazoendelea za serikali ya Tanzania na washirika wake utasaidia watoto wengi wa kike kuweza kushiriki masomo bila kikwazo chochote 

Ameongeza kuwa uandikishaji wa wavulana na wasichana kwenye shule za msingi ni karibu sawa, lakini viwango vya kumaliza sekondari kwa wasichana vinarudi nyuma

Bi. Kate amesema ndoa za utotoni na mimba - na kutothamini mafanikio ya wasichana - ni vikwazo. Miongoni mwa vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya 20-24, moja ya tano wa wasichana na theluthi moja ya wavulana humaliza sekondari.

Shule ya sekondari ya Loyola iliopo Manispaa ya Ubungo katika mtaa wa Mabibo farasi jijini Dar es Salaam inalenga kuwasaida watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao familia zao hazina uwezo wa kumudu mahitaji yao ya elimu, lakini Lengo kuu la Mpango wa USAID ASHA jijini Dar es Salaam ni kuongeza idadi ya vijana wa Kitanzania hasa wasichana waishio katika mazingira magumu kupata elimu bora

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, naibu katibu mkuu wa Wizara hiyo Prof. James Mdoe amesema ujenzi wa mabweni haya mapya utaongeza uandikishwaji na kubakia wa wasichana waishio katika mazingira magumu katika shule ya sekondari ya Loyola na kupunguza athari wanazokabiliana nazo kila siku kwenda na kurudi shuleni

Ameongeza kuwa moja ya malengo ya wizara ni kuhakikisha vijana wanapata elimu bora hutengeneza fursa za kujihusisha na kupata maarifa na ujuzi muhimu

Matokeo yake, vijana wataendeleza ustawi wa muda mrefu wa Tanzania huku wakitengeneza nchi kwa mustakabali wanaoutamani.Akizungumza katika hafla hiyo

Kwa kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo wakiwa shuleni na kwenye jamii yao, wasichana wa Kitanzania wana uwezo mkubwa wa kumaliza elimu yao, kuwa na afya bora, kupata ajira, na kupunguza umaskini katika jamii

Mkuu wa Shule hiyo, Fr. Martin Waweru alisema sababu ya shule hiyo kuanzisha bweni ni kuondoka a na changamoto za malezi na makuzi ya wanafunzi ikiwamo ugumu wa usafiri, mazingira ya mtaani na ushirikiano duni kwa baadhi ya wazazi na walezi na kwamba bweni litakuwa na uwezo wa kuhudumia wasichana 453.

Aidha, Fr. Waweru aliiomba serikali kuboresha mfumo wa ushindani akisema hautoi uwiano sawa hasa kwa shule za bweni, wanafunzi wengi na kwamba kuwepo bei elekezi ya vitabu na  vifaa vya kitaaluma.


Post a Comment

0 Comments

THBUB YAHIMIZA WANANCHI NA WATUMISHI KUHESHIMU MISINGI YA UTAWALA BORA