UBUNIFU WA WANAFUNZI LOYOLA WAIPAISHA TANZANIA KATIKA TEKNOLOJIA



Mkuu wa shule ya Sekondari Loyola Baba Martin Waweru.


Wanafunzi wabunifu wa shule ya Sekondari Loyola wakionesha moja ya ubunifu wao katika uzinduzi wa bweni la wasichana la shule hiyo.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MKUU wa shule ya sekondari Loyola Baba Martin Waweru amesema wanafunzi wenye vipaji wana nafasi kubwa ya kubadili mfumo wao maisha baada ya masomo katika shule hiyo kutoka na malezi wanayopata kupitia mafunzo ya teknohama

Ameyasema hayo wakati uzinduzi wa Bweni la wasichana shuleni hapo Jijini Dar Es Salaam wakati wazazi walipotembelea darasa maalumu shuleni hapo kuangalia kazi za ubunifu kutoka kwa wanafunzi

Katika darasa hilo wazazi walijionea ubunifu katika nyanja mbalimbali za mawasiliano pamoja na uzalishaji wa bidhaa za  ujasiriamali na kuuliza maswali ambayo walijibiwa kwa ufasaha na kuonesha baadhi ya vifaa vilivyobuniwa na vijana hao

Akizungumza katika uzinduzi wa Bweni hilo la Wasichana mkuu huyo wa shule Baba Waweru ameshukuru wazazi na wadau wote wa elimu ambao wameshiriki kikamilifu katika ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi na kipekee ametoa shukrani kwa serikali ya Tanzania pamoja na Shirika la Kimataifa kutoka Marekani (USAID) kwa mchango wake mkubwa katika elimu nchini na kuongeza kuwa malengo ya shule ya Loyola ni kuboresha matokeo ya elimu kwa vijana hususani wasichana kwa kuwa Mara nyingi upatikanaji wa Elimu unaweza kukatizwa na kutokana na changamoto ya wasichana kukosa sehemu salama ya kujigunzia, hivyo kwa kukamilisha ujenzi huo ni mafanikio makubwa sana katika sekta ya elimu

Vilevile mkuu huyo ametoa wito kwa wanafunzi pamoja na wazazi kushiriki kwa pamoja katika maendeleo ya elimu kwa vijana kutoka na uwepo wa masomo ya teknohama katika shule hiyo ambayo yatawasaidia kutatua changamoto mbalimbali 

Baba Waweru ameongeza kuwa sababu ya shule hiyo kuanzisha bweni ni kuondoka a na changamoto za malezi na makuzi ya wanafunzi ikiwamo ugumu wa usafiri, mazingira ya mtaani na ushirikiano duni kwa baadhi ya wazazi na walezi na kwamba bweni litakuwa na uwezo wa kuhudumia wasichana 453.

Aidha, Baba Waweru aliiomba serikali kuboresha mfumo wa ushindani akisema hautoi uwiano sawa hasa kwa shule za bweni, wanafunzi wengi na kwamba kuwepo bei elekezi ya vitabu na  vifaa vya kitaaluma

Ameongeza kuwa moja ya malengo ya shule ni kuhakikisha vijana wanapata elimu bora hutengeneza fursa za kujihusisha na kupata maarifa na ujuzi muhimu

Matokeo yake, vijana wataendeleza ustawi wa muda mrefu wa Tanzania huku wakitengeneza nchi kwa mustakabali wanaoutamani katika maisha ya baadae

Kwa kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo wakiwa shuleni na kwenye jamii, wasichana wa Kitanzania wana uwezo mkubwa wa kumaliza elimu yao, kuwa na afya bora, kupata ajira, na kupunguza 





Post a Comment

0 Comments

THBUB YAHIMIZA WANANCHI NA WATUMISHI KUHESHIMU MISINGI YA UTAWALA BORA