WAOMBA RAIS SAMIA KUINGILIA MGOGORO WA NARCO

Mmiliki wa kitalu namba 10, Hashim Kuhorela akizungumza na waaandishi wa habari (hawapi pichani).

Na Mwandishi wetu, Dodoma

WAMILIKI wa vitalu vya Shirika la Ranchi la Taifa (NARCO), wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, kuingilia Kati na kuunda Tume kwa ajili ya kufuatilia mgogoro wa wawekezaji na wananchi katika Kitalu namba 10 cha Kagoma Complex Muleba, uliodumu tangu mwaka 2008.

Mwekezaji Hashim Luhorela, ambaye ni mmoja wa wamiliki wa vitalu hivyo anayemiliki katika kitalu namba 10, alizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana ambapo alisema kuwa mgororo huo umedumu kwa muda mrefu na sasa bado haujapatiwa ufumbuzi dhidi ya wawekezaji wa vitalu na jamii inayozunguka katika maeneo
hayo.

Alifafanua zaidi ya kuwa mgogoro huo,umezidi kuwa mkubwa hali inayosababisha uharibifu wa mali ndani ya Vitalu ambao unachangia hali
ya uwekezaji kuwa mbaya katika vitalu hivyo,ikiwemo kuhatarisha usalama na mazingira ya wawekezaji.

 “Tunaomba Rais uunde tume ambayo itafuatilia mgogoro huo,tunahitaji kuona unakwisha ili wawekezaji waweze kutimiza majukumu yao kirahisi bila bugudhi yoyote na kujiinua kiuchumi,”alisema Luhorela.

Hali hiyo inajitokeza wakati Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia ikijipambania kuwalinda wawekezaji na kuwahamasisha kuwekeza nchini wakiwemo wawekezaji wa ndani.

Luhorela aliishkuru serikali kwa kuendelea kuwalinda wawekezaji wa ndani na nje ili kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, taratibu,kanuni na miongozo ya nchi na kuongeza wataendelea kushirikiana ili kuhakikisha suala hilo linafikia ukomo.

Alisema wawekezaji katika vitalu hivyo wanalengo la kuboresha vitalu hivyo ambavyo vinafaida kubwa kwa jamii kutokana na ufugaji wanaofanya.

"Naanzia pale mgogoro ulipozidi kuwa mkubwa na uharibifu wa mali ndani ya vitalu kuwa wa kutisha na hali kuwa mbaya zaidi na wakati huo huo viongozi wenye mamlaka katika wilaya husika ya Muleba, na viongozi wa mkoa wa Kagera,....

"Mheshimiwa Rais tumendelea kuwa wavumilivu tukijua tutapata msaada serikalini bila mafanikio yoyote mwaka 2013, Nilipeleka shauri hili mahakamani baada ya kuona hali inapitiliza ni shauri no 2/2013,"alisema.

Alifafanua kuwa baada ya shauri hili kusikilizwa lilitolewa uamuzi na  Jaji Machi 10, 2017 wananchi hao wakiwa wameshindwa na kutakiwa kupisha ndani ya kitalu hicho.

Alisema wakati wa zoezi hilo wananchi hao walioaminishwa na viongozi wa kisiasa sasa hawana msaada wowote wanaugulia maumivu wako wanalaani serikali yako tukufu wakati wewe hujawatuma kuwadhuru raia wasio na hatia, ukitaka kujiridhisha unda tume ndogo ujue madhara waliyoyapata raia wako ambao walipotoshwa.

Post a Comment

0 Comments

UTALII NA MADINI ZINACHANGIA KWA PAMOJA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA