DIANA: NILICHOMWA MIONZI 28 TANGU MWAKA 2019 HADI LEO SIUMWI POPOTE

Mkazi wa Arusha Diana IJengo mwenye tatizo la ugonjwa wa sarataSa ya sikio la kati.

Na Asha Mwakyonde

" KUNA moja ya Hospitali kubwa ya mkoani Dar es salaam  nilienda kupima wakanificha  majibu yangu baada ya kupima lakini baadae nilimpata daktari ambaye ni rafiki ya mama yangu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Moshi (KCMC), aliniambia nina Saratani ya sikio Sehemu ya kati (Middle Ear),ila sikuridhika nae nikampa daktari Salumu wa jijini Dar es Salaam," ameongeza.

"Alinisomea yale majibu akaniambia nina ugonjwa wa Saratani ya sikio ambapo kulikuwa na nyama iliyoota ndani ya sikio hili. Kiukweli sikutaka kuamini nilipokea majibu hayo nikiwa kwenye bajaji nililia na baadae nikaona kulia haisaidii chochote," hayo ni maneno ya Mkazi wa Arusha Diana Ijengo akisimulia alivyoanza kuugua ugonjwa wa Saratani ya sikio la kati.

Akizungumza na Tanzania na Habari Blog katika mahojiano Diana amesema daktari wa Hospitali ya Muhimbili hakuweka wazi kuwa anatatizo gani na badala yake akamwambia sikio lake lina nyama na si Saratani.

Amesema Februari mwaka 2018 ndio aligundua kuwa ana ugonjwa wa Saratani ya sikio la kati na kwamba alipata mwamuko wa kwenda hopitali kupima.

Diana amefafanua kuwa mwaka 2017 kabla ya kujua ana tatizo gani alijiona yupo tofauti na hali yake ya kawaida aliyoizoea siku zote.

Ameongeza kuwa alichelewa kwenda hopitali ambapo tayari Saratani hiyo ikiwa katika hatua ya nne.

DALILI

Akizungumzia dalili alizoziona na kumsababishia aende hospitali kupima Diana amesema baadhi ya dalili hizo ni wakati akila chakula alikuwa akipaliwa, kutapika na matapishi kutokea puani.

"Nilikuwa sisikii vizuri pia nilikuja kusikia maumivu makali  kwenye paji la uso,sikio lilikuwa linawasha sana na kutoa uchafu wa wenye rangi ya kahawia (brown), wenye harufu, maskio kupiga kelele nilikuwa  nahisi kama mapigo ya moyo yanadundia kichwani," amesema.

CHANGAMOTO

Amesema awali alikuwa akikutana na changamoto mbalimbali ikiwamo kupata maumivu makali, sikio Kutoa usaa,damu na maji yenye harufu.  

"Nlikuwa siwezi kula vizuri kwaajili ya kupaliwa, sikio pia kwa upande wa  nyuma lilikuwa limetoboka nyama inaonekana, usiku silali kwajili ya maumivu changamoto ni nyingi sana ila namshukuru Mungu kwa yote," amesema.

MILA POTOFU

Diana amesemakuwa baadhi ya wanajamii waliomzunguka walisema haugui  ugonjwa wa saratani bali amerongwa kwa kuzaa na mume wa mtu.

"Mume wangu sio mume wa mtu na wala hana mtoto wa nje zaidi wa huyu wangu tuliyezaa naye ambaye ana umuri wa mika mitatu," amesema.

ANATOA WITO KWA JAMII

Diana ameitakajamii jamii iondokane na imani potofu za kuhisi mgonjwa amerogwa na badala yake waende kupata vipimo kutoka kwa Walaamu wa afya.

 Amefafanua kuwa  jamii pia itambue kuwa ugonjwa wa saratani unatibika ikiwa umewai na kwamba na hata ikicheleweshwa inatibika kwa asilimia kidogo tofauti na ikiwa mtu bado hajaanza kupata tiba.

"Niliambiwa ugonjwa umefika hatua ya mwisho tena imefika hadi kwenye  mfupa wa mawasiliano kichwani karibu na ubongo na hospital nilichomwa mionzi 28 toka mwaka 2019 mwezi wa11 hadi  leo sjawahi kuumwa popote," ameeleza Diana.

Amesema kwa sasa usaa na damu hamna tena koo limetulia na anakula vizuri  na kwamba alivyorudi kiliniki  aliambiwa arudi  nyumbn kwa sababu hawezi siwezi kupona kwani ugonjwa upo stage mbaya hivyo yeye ni tibaa shufaa (palliative care).

"Sifanani na mgonjwa kwa kuwa  nipo mzima nina nguvu nafanya kazi nimeajiriwa na nina mtoto sasa  ana umri wa miaka 3.Naishauri jamii iache kunyanyapaa wagonjwa na wasiache kuwapeleka wagonjwa hospitali, wafuate vile wanavyoambiwa na madaktari  na kuwajali  wagonjwa kiroho na kwakuwapatia mlo kamili, maji ya kutosha pamoja na juice za kuongeza damu," amesema.


Post a Comment

0 Comments

UDOSO SCHOLARSHIP FUND YAZINDULIWA