DK.SICHALWE AAGIZA WATUMISHI WA AFYA KUFUATILIA WANAOHISIWA NA DALILI ZA MAGONJWA YANAYOATHIRI MFUMO WA NJIA YA HEWA, WATOTO NAO WAMO


 Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifello Sichalwe

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

SERIKALK kupitia Wizara ya Afya imewaagiza Watumishi wa afya kuimarisha ufuatiliaji wa wagonjwa wote wanaohisiwa kuwa na dalili za magonjwa yanayoathiri mfumo wa njia  hewa na kwamba watoto chini ya miaka 12 takwimu zilizokusanywa  na Wataalam  Mkoa wa Dar es Salaam zinaonesha sampuli  16 kati 123 zilionesha watoto hao wana mafua.

Pia Wizara hiyo inatoa wito kwa watu wote wenye dalili za homa, kikoozi na mafua kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wapate matibabu sahihi na kutotumia dawa bila kuandikiwa na Wataalam wa afya.

Agizo hilo limetolewa leo Machi 30, 2022, jijini hapa kupitia taarifa iliyotolewa na  Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Aifello Sichalwe kuhusu tamko la ongezeko la watu wenye dalili za magonjwa yanayo athiri mfumo wa njia ya  hewa nchini amewataka watumishi hao kuendelea kuchukua sampuli kwa wagonjwa wote wenye  dalili za magonjwa yanayo athiri
mfumo wa njia ya hewa.

Pia amewasisitiza waendelea kutoa elimu ya afya kuhusiana na magonjwa hayo yanayo athiri mfumo wa hewa kwa
kutumia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari,mitandao ya kijamii na vituo vya
 hutoleahuduma.

"Wizara ina shauri wananchi kuendelea kujitokeza kupata chanjovya UVIKO-19 katika vituo vya kutolea hudumazva
afya,na inawakumbusha kukamilisha dozi ili kupata kingakamili," amesema Dk. Sichalwe.

Dk.Sichalwe ameongeza kuwa kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa wagonjwa wizara hiyo imechambua taarifa inzozipokea  kila siku  na kubaini uwepo wa  ongezeko la watu dalili  za homa, kuhohoa, mafua, kubanwa kifua na maumivu makali ya mwili kwa kipindi cha Disemba 2021 hadi Machi 25 mwaka huu.

" Ongezeko hili limekuwa  limekuwa likitokea katika kipindi cha mwishoni na mwanzoni mwa mwaka kwa miaka mitatu mfulilizo ambapo limekuwa likipungua  mwaka hadi mwaka," amesema mganga huyo Mkuu wa Serikali.

Amefafanua kuwa kwa mwaka 2019 hadi 2020 kulikuwa na jumla ya wagonjwa 9,804,356 mwaka 2020 hadi 2021 na kwamba wagonjwa 8,503,409 na mwaka 2021 hadi 2022, wagonjwa 3,316,884 takwimu hizo ni za miezi minne Disemba hadi Machi kwa mwaka husika.

Dk. Sichalwe ameeleza kuwa ufuatiliaji wa mafuta makali (Influenza), unaofanywa katika mika 14 kwenye hospitali 18 nchini umebaini uwepo wa kirusi Cha Influenza ambapo kati ya sampuli 1,843 zilipimwa kwa kipindi cha Disemba 12, 2021 hadi Machi 13 mwaka huu na kwamba jumla ya sampuli 55 sawa na asilimia 3 zilionekana kuwa na virusi vya Influenza A vinavyosababisha mafua makali na Nimonia.

" Kirusi hiki cha kimekuwepo hapa nchini kwa muda mrefu na sio kirusi kipya. Kwa ujumla kiwango cha maambukizi cha kirusi hiki kinaonesha kupungua ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo kilikuwa cha wastani wa aslimia 5 hadi 6," amesema Dk. Sichalwe.

Amesisitiza kuwa wizara ina utaratibu wa kufuatilia taarifa magonjwa hususan yale ya milipuko pamoja na matukio yanayo athiri afya za binadamu hapa nchini na kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti au kupubguza kwa kiasi kikubwa madhara yanayoweza kutokea.

" Katika ufuatiliaji huo jumla ya sampuli 123 zilizochukuliwa kutokakaa watoto wenye tajwa  kutoka vituo vilivyokusanywa kwa ajili ya vipimo ya maabara matokeo yalionesha sampuli 16 kati ya 123 sawa na asilimia 13 ya sampuli zote zilikuwa na  virusi vya  mafua Influenza A na sampuli zote hazikuwa na UVIKO-19. 

Amefafanua kuwa kiwango hicho cha asilimia13 ni kikubwa ikilinganishwa na kile cha wastani asilimia 5 hadi 6 ambacho kumekuwapo hapa nchini kwa muda mrefu.

Dk.Sichalwe amesema hall hiyo imejitokeza wakati bado kuna UVIKO-19 nchini ambapo takwimu za matokeo ya upimaji katika kipindi cha Januari hadi Machi 20, zimeonesha kupungua kwa visa kutoka wastani 138 kwa siku Disemba 2021 hadi visa vitano kwa siku Machi 2022.









Post a Comment

0 Comments

UDOSO SCHOLARSHIP FUND YAZINDULIWA