Akifungua mafunzo hayo leo jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jimy Yonazi amewataka Wakuu hao wa upelelezi kutumia mafunzo waliyopewa kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao kwa kujifunza zaidi ili wawe wabobezi.
Hata hivyo amewataka Wakuu hao wa upelelezi kuhakikisha wanawalinda wananchi wote kwaajili ya usalama wao na mali zao kwa maslahi mapana ya Taifa.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini,Kamishna Camilius Wambura( DCI)amesema mafunzo hayo yatakuwa ni chachu kwa Jeshi la Polisi na malengo ni kila Askari awe na elimu kuhusu makosa ya mtandao ambayo kwa sasa yameshika kasi.
Awali,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP,Joshua Mwangasa amesema tayari wameshaanza mradi wa utekelezaji wa kanda sita za maabara za kiuchunguzi ili kupanua wigo wa kiuchunguzi nchini kwani awali walikuwa na maabara moja tu.
0 Comments